WENYE "VIPARA" WAUAWA, WADAIWA KUWA WANA "DHAHABU" NDANI YA VICHWA VYAO.

 Baadhi ya wenye vipara wamekuwa wakiuawa nchini Msumbiji kutokana na imani za kishirikina ambapo inaaminika kufanya hivyo ni kijipatia utajiri wa haraka na wengine kudai vichwa vya watu hao vina dhahabu. 
Hadi sasa Polisi katika jimbo la Zambezia nchini "Msumbiji" wamewakamata watu wa nne kwa kuhusika na mauaji ya watu wenye vipara. Pia wanaendelea na uchunguzi huku wakifuatilia zaidi kujua nani anachochea mauaji hayo. 
Waganga wa kienyeji wamekuwa wakidaiwa kusambaza habari zisizo na ukweli kwamba vichwa vya watu wenye vipara vimekuwa na dhahabu. 
Pia Polisi wamekuwa wakichunguza mauaji ya albino ambao wamekuwa wakikatwa viongo vyao vya mwili, na kutumika katika masuala ya imani za kishirikina.
By CHAX C


Comments