TATIZO LA FANGASI (MAAMBUKIZI, DALILI) NA MATIBABU YAKE (NAMNA YA KUJIKINGA).

Huu ni muendelezo kwenye maada ya CHANZO CHA FANGASI NA MATIBABU YAKE, ambayo imegawanyika katika sehemu muhimu ambazo ni; sababu zinazozababisha Fangasi, Dalili za ugonjwa wa Fangasi, Tiba gani itatumika kuwaua Fangasi na namna ya kujikinga dhidi ya Fangasi.
Leo tunaendelea na muendelezo wa kuhusu TATIZO LA FANGASI (Kinachosababisha,Mazingira ,Maambukizi na Dalili za Fangasi) na MATIBABU YAKE (Tiba na Namna ya Kujikinga)
katika hali ya kawaida, ngozi ya binadamu huhufadhi kiasi kidogo cha Fangasi hawa kunufaisha pande mbili ambazo ni “mhusika” pamoja na “wadudu wenyewe” kila upande unapata faida kutoka kwa mwenzake (PARASITISM). Lakini madhara hutokea wakati mwingine kama Fangasi watazaliana na kuongezeka zaidi.
wapo Fangasi wa aina nyingi lakini kwenye mashambulizi mengi mfano "Tinea corporis" ni aina ya Fangasi wanaoathiri (kushambulia) ngozi zaidi ya sehemu za mikono, miguu na sehemu za laini katika ngozi (Glagrous skin). Nyingine ni "Candida albicans" ndiyo huhusika zaidi.

Madhara ya Fangasi yanatibika na kupona ikiwa matibabu sahihi yatapatikana kwa wakati. Hata hivyo, Fangasi wasipotibiwa huongezeka na kuwa tishio kwa maisha ya mgonjwa hasa kwa mwenye upungufu wa kinga mwilini kama vile muathirika wa UKIMWI.
          KINACHOSABABISHA
Maambukizi ya Fangasi hutokea sehemu yoyote mwilini lakini mara nyingi huvamia zaidi eneo ambalo nyama zinakutana kwenye mikunjo, vidonda, michubuko, wakati mwingine nyama zinaposuguana. Sehemu hizo ni kama kwapani,Mdomoni, tumbo linapokutana na sehemu ya juu ya paja na maeneo ya katikati ya vidole vya mikono na miguu.

Vimelea hivi na kustawi zaidi sehemu zenye joto, unyevu na nyakati za kutoka jasho kwa wingi.
Katika hali ya kawaida ngozi huzuia mwili usivamiwe na viumbe wavamizi wanaopenya na kuingia mwilini.
Inapotokea mkato au mpasuko wowote katika sehemu ya juu ya ngozi unaoruhusu kuwa na uwazi. Eneo ndani yake huwa wazi na kusababisha Fangasi kupenya na kuleta madhara.
                MAZINGIRA.
Fangasi wanapopata mazingira mazuri ya kuishi huathiri mwili kwa kiasi kikubwa, mazingira hayo ni joto, unyevu,uchafu wa mwili au uvaaji wa mavazi yanayobana. Mazingira zaidi ya haya yanaweza kusababisha uvamizi wa Fangasi kama vile ukitumia vidonge au tiba nyingine kwa muda mrefu.
Dawa hizo ni kama za kuua Bakteria (Antibiotics), na dawa za kupanga uzazi. Unapotumia dawa hizi ni vema kufuatilia kwa karibu hali ya ngozi yako ili kubaini uvamizi wa Fangasi.

               MAAMBUKIZI
  • Kupitia kugusana na mtu aliyeathirika na Ugonjwa wa Fangasi (Body Contact)
  • Kupitia kuambukizwa na Wanyama kama vile mbwa n.k (Animal to Human transmission)
  • Kugusa vitu ambavyo vina vimelea vya Fangasi kama vile nywele, nyusi za muathirika wa Fangasi.(Touching inanimate Objects)
  • Kuchangia nguo na muathirika wa Fangasi.
  • Kufanya Mapenzi na muathirika wa Fangasi (Sexual Intercoarse) au Sharing kiss with an infected victim. n.k
                 DALILI.
Uvamizi wa Fangasi una dalili mbalimbali kukingana na sehemu ya mwili iliyoathirika ambazo ni pamoja na kutokwa vipele (vinavyowasha na ngozi kuwa nyekundu), mabaka mekundu, kutokwa vumbi jeupe sehemu iliyoathirika.
Wakati mwingine kutokwa magamba, ngozi kupasukapasuka, maumivu na ukomavu wa misuli, utando mweupe na mbabuko, pamoja na vidonda vyeupe au vyekundu midomoni.
                KUGUNDUA TATIZO (TIBA)
Ugunduzi wa tatizo hufahamika baada ya uchunguzi wa Daktari kwa kuangalia sehemu iliyoathirika au kupitia kipimo.
Sehemu ndogo ya ngozi, kucha au maeneo ya chini ya nywele katika sehemu iliyoathirika huchukuliwa na kufanyiwa kipimo Maabara (Laboratory). Mara baada ya tatizo kugundulika na Daktari huchunguza zaidi ili kufahamu chanzo cha Fangasi kwa mhusika.
Vyanzo ambavyo vinahusika ni kama mabadiliko ya hali ya Usafi wa mwili au kisukari na utunzaji wa ngozi.
Matibabu ya Fangasi wa ngozi huwa ni rahisi mgonjwa anatumia dawa za kukausha ngozi, Krimu za Fangasi, Mafuta au Losheni ili kupaka sehemu iliyoathirika.
Iwapo madhara ya Fangasi ni makubwa au hayajapona kwa Dawa za awali basi Daktari humpatia mgonjwa Dawa zaidi kwa njia ya mdomo au sindano.
                    NAMNA YA KUJIKINGA
Zipo njia mbalimbali za kujikinga dhidi ya uvamizi wa Fangasi ambazo ni pamoja na
  • Uvaaji wa nguo zilizokauka kikamilifu zinazoweza kunyonya unyevu wa ngozi yako.
  • Usivae nguo zinazobana kwa muda mrefu.
  • Hakikisha hali ya Usafi sehemu zinazokuza Fangasi kama Kwapani, sehemu kati ya tumbo na paja, katikati ya vidole na sehemu nyingine zote zinazojulikana kwa kukuza Fangasi.
  • Pia ni vyema kukausha sehemu zote za mwili zenye mikunjo haswa kwa watu wanene, kuoga na kujikausha vizuri kila baada ya kazi zilizokutoa jasho, kuvaa viatu vya wazi nyakati za joto na kubadili soksi na nguo za ndani mara kwa mara.
  • Kwa watu wazima Fangasi sio tatizo kubwa la kutishia uhai kwani hutibiwa na kupona. Maambukizi ya Fangasi ni hatari zaidi kwa wazee na watoto wadogo pamoja na wenye upungufu wa kinga mwilini kama vile muathirika wa UKIMWI.
  • Linakuwa tatizo kubwa kwa makundi haya kwa vile madhara husambaa sehemu nyingine za mwili ikiwamo Koromeo, Valve za Moyo, Tumboni, Ini na kwenye Mapafu. Ni muhimu kuwahi Matibabu mapema pale unapogundua ugonjwa kwani kadri unapowahi kutibu ndivyo unavyopona mapema.
  •   Iwapo hali ya Muwasho inaambatana na maumivu ya tumbo au homa kali basi Wahi haraka hospitali.
Imeandaliwa na CHAX C 
**ASANTENI SANA**

Comments