…..WAKATI MWINGINE LIKE FATHER UNLIKE SON. …
Ndani ya mwezi ulioisha manzoni zilienea taarifa juu
ya ziara ya mwanasoka wa zamani wa vilabu vya Manchester United, Real Madrid,
LA Galaxy,PSG pamoja na timu ya taifa ya England DAVID BECKHAM… taarifa za
uwepo wake hapa bongo zilianza kusambaa mara baada ya picha na vipande vya
video zilizorekodiwa kwa siri pale airport ya JKIA kuzagaa katika mitandao
mbalimbali ya kijamii ikiwemo whatsapp, baadaye kwa picha mitandao ya habari ya
uingereza likiwemo gazeti la daily mail ilithibitisha kuwa Becks alikuwa
akifanya ziara ya kitalii barani Afrika pasipo kutanabaisha nchi gani akiwa na
watoto wake wawili Brooklyn na Harper seven, baadaye yeye mwenyewe aliposti
picha mtandaoni akionekana kuwa mbugani na wabongo wakathibitisha kuwa huenda
“”Bishoo “huyo yupo mbuga za wanyama za Serengeti …sasa bana kuna picha moja
Bekham amepiga akiwa na maaskari wanyamapori wawili… pasina shaka mpiga picha
wao alikuwa Brooklyn… unampata vizuri huyu dogo???
Beckaham akiwa na Maaskari wanyamapoli wa mbuga za Serengeti..mapema mwezi ulioisha |
Huyu ni mtoto wa kwanza kati ya wanne wa Beckham
ambao alizaa na mkewe mwanamuziki wa zamani na mwanamitindo Victoria Adams
…dogo alizaliwa tarehe 9 machi 1999 pale Winchester -England,mimba yake
ilitungwa kwenye fukwe za kifahari
zinazopatikana Brooklyn katika jiji la New York -Marekani… Inasemekana Bekham
alienda kule kujipumzisha na aliyekuwa mpenzi wake wakati ule kabla hawajaoana
rasmi Victoria…mshikaji alienda kule ili kupunguza stress baada ya kuonyeshwa
kadi nyekundu kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Argentina
huko St ettiene -ufaransa na kushuhudia England ikifungwa mechi ile kwa matuta
na kutupwa nje ya michuano hiyo mikubwa kwenye historia ya soka duniani…
Beckham alilaumiwa sana na mashabiki pamoja na vyombo vya habari vya uingereza
kwa tukio la kijinga la kumpiga teke kwa makusudi nahodha wa Argentina wa
wakati ule Diego Simeone(kocha wa sasa wa atletico Madrid) na kupelekea kadi hiyo ya kizembe iliyopelekea
wachezaji wenzie kumaliza wakiwa pungufu… …kwa vile mimba ya dogo huyo
ilitengenezwa hapo Brooklyn -New York City jamaa alivutiwa kumuita mwanaye
jina la Brooklyn Beckham…
Beckham akiwa na Brooklyn..picha hii walipiga wakiwa mbuga za wanyama za Serengeti.
|
Katika maisha ni kawaida kuwaona watoto wakikua na
kufanya kile ambacho wazazi wao walifanya na kikawapa umaarufu ….ni kweli
kabisa watoto hasa wa kiume wengi wao huishi kufata nyayo za baba zao (Like
father like son) kuthibitisha hilo hapa bongo tunao akina ridhiwani
kikwete,january makamba, Mrisho Ngassa, himid mao… salum abubakar (sure boy) na wengineo.. Ukienda kenya wapo akina Uhuru
Kenyatta, Raila Odinga na Victor Wanyama.. Gabon kuna Ali Bongo… Ghana kuna
wale Andre na Jordan Ayew… wote hawa niliokutajia walifuata mule mule baba zao
walipitia na kufkia wengne waka “achieve “ zaidi… sijajua hili ni kwa nini lakini
nadhani ni kwa sababu ya mfumo wa maisha ya tabaka la kati kwa waafrika …..Hali
ni tofauti kwa wenzetu WAZUNGU, ni nadra sana kumkuta mtoto wa kiume wa kizungu
akiishi kupenda na kufanikiwa kupitia kile alichofanya baba yake… unahisi ni
kwa nini?? …ni kwa sababu watoto wale wengi wao wanakuwa dhaifu wa fikra na
akili za kiutafutaji kama walivyokuwa wazazi wao… mtoto wa kizungu aliyetokea
familia tajiri hapendi kujihangaisha au kuhustle maadamu anaona mali alizochuma
baba yake zinatosha na ndio zitakuwa kianzio cha yeye kufanya mitikasi
atakayoona inamfaa tofauti na aliyoitumia baba yake…
Kwa sasa Brooklyn Beckham ana miaka 18,kama
alivyokuwa baba yake tulitegemea angekuja kuwa kiungo bora wa kati na pembeni
kulia… pengine labda akatufungia magoli maridadi ya mipira iliyokufa kama
ambavyo waingereza walitokwa na machozi ya furaha jioni ya tarehe 6 October
2001 kwenye dimba la Villa Park pale ambapo shuti Lake la faulo ya umbali wa
karibu mita 37 lilijaa wavuni dakika za lala salama na kuipa England tiketi ya
kushiriki kombe la dunia mwaka uliofuata kwenye nchi za Korea na Japan… Beckham
alikuwa na bidii haswa uwanjani, angepiga faulo na kona zotepeke take angehama
pembeni ya uwanja na kusogea katikati ilimradi kwa bidiiile alitaka kutengeneza
jina lake na kupiga PESA ndani na nje ya uwanja,nadhani ilichagizwa na aina ya
maisha ya kawaida aliyokulia kwao,ikumbukwe jamaa ni mtoto pekee wa kiume Kwao
… …..lakini hali ni tofauti kwa Brooklyn,dogo ni “mtoto wa Mama” haswa ….mpaka
sasa haijulikani kipaji chake haswa ni nini….Mwaka 2008 wakati anaitumikia LA
Galaxy Beckham alimtambulisha dogo huyo kwa nyota wa kikapu wa timu ya LA
Lakers ambayo Ilikuwa inatoka mtaani kwao walipoishi mjini Los Angeles….bekham
alifanya hivi baada ya dogo huyo kumshinikiza kuwa anapenda mpira wa kikapu na
anataka ajifunze hivyo yeye kama mzazi akatumia ushawishi wake kumpeleka
kuonana na akina Kobe Bryant ili apate inspiration na exposure juu ya mchezo
ulokuwa ukimvutia.. Lakini dogo alibadirika ghafla na kuacha kuufutilia tena
mchezo huo ….akavutiwa na uigizaji kisa ukaribu wa familia ya Beckham na
familia ya Thom Cruise. ..Hakuishia hapo akaona isiwe tabu akaamua kujifunza
kucheza soka,,, nadhani ilikuwa baada ya kuona wivu juu ya medali nyingi ambazo
baba yake alishinda kwenye soka…. Ilifikia baba yake akampeleka kufanya
majaribio ya kujiunga na academy ya arsenal kati ya mwaka 2011-2013 lakini mzee
Wenger humdanganyi kitu kuhusu kipaji halisi cha soka na alimpiga chini dogo
huyo licha ya ukaribu alionao na baba yake …akapelekwa tena kwingne… zamu hii
ilikuwa ni Manchester United timu ambayo ilimtambulisha baba yake katika
ulimwengu wa soka …kama iivyotarajiwa na wengi alishindwa kusajiliwa kutokana
na miguu yake kushindwa kulishawishi jopo la makocha wa timu za vijana wa timu
ile akiwemo Nicky Butt ambaye alikulia pamoja na Beckham katika kizazi cha
iliyotoka kuwa timu ya vijana ya Man United (Class Of 92) hadi kizazi cha
mafanikio cha Alex Ferguson akiwa pamoja pia na akina Garry na Phil Neville,,
Paul scholes na Ryan Giggs…. .
Katika umri wa miaka 16 tu tiyari Brooklyn
alishaandikwa na magazeti ya udaku akihusishwa na kujirusha na mademu kwenye
kumbi za starehe… .Leo hii dogo akiwa na umri wa miaka 18 tiyari amejichora
tatoo mkononi …alishaanza kuibia kupiga deal za mitindo… anavuta sigara…
ikumbukwe Kyllian Mbappe ameandika record yake katika michuano ya UeFa mwaka
huu akiwa na miaka sawa na Brooklyn na ndio Kwanzaa akina Real madrid na
Arsenal wanapandiana dau ili kupata huduma yake……. Kama kumbukumbu hazidanganyi
dunia ya soka ilimtambua Neymar kuwa mchezaji mzuri wa baadaye akiwa na miaka
17 tu, Messi yeye tulimtambua akiwa na miaka 16 tu sawa na Martin Odegaard, CR7
yeye alishaonekana na baiskeli zake miguuni akiwa na miaka 18. ..mwaka jana
mwishoni aliibuka Karamoko Dembele akiwa na miaka 13 pale Celtic FC ya Scotland
akishacheza mechi yake ya kwanza na timu ya under 19(kama humjui ingia YouTube
ukaone balaa lake) …hao wote wametokea familia za kawaida na wengine maskini na
kujituma kwao kumewafikisha juu kisoka duniani…. Lakini nina wasiwasi kama
Brooklyn Beckham atakuja kuwa mwanasoka NGULI kama baba yake, ..kwa huu umri
wake tungekuwa tushaona maajabu fulani kwenye miguu yake…. Haswa ukizingatiwa
kuwa vipaji halisi vya soka vilijulikana wakati wa umri kama huu …leo hii timu
ya taifa ya England chini ya umri wa miaka ishirini inafuzu robo fainali ya michuano ya dunia huku ile Chini ya miaka ishirini namoja ipo kambini kujiandaa
na michuono ya euro kwa ngazi hiyo… unafikiri Brooklyn yumo kwenye hizo timu….
.hapana yeye yuko Tanzania akifurahia kuwaona simba na chui huku akifurahia
kumpiga picha Baba yake akiwa na askari wanyamapori wa kitanzania… .unadhani
siku moja labda Brooklyn atakuja kucheza Man United au Real Madrid?????? Ngoja nikuambie kitu,nilishawahi kuangalia
mechi moja mwaka juzi(kupitia luninga),mechi ya hisani
iliyoandaliwa na David Beckham kwa ajili ya kuchangia watoto maskini ,ilhusisha
wachezaji wa zamani wa Man United dhidi
ya wengne waliowahi kucheza soka enzi moja na Beckham, Brooklyn
aliingizwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya baba yake …nikuambie kitu yule
dogo hana jipya katika miguu yake
uchezaji wake haukutofautiana na wale maveterani waliokuwemo mle ndani ….kwa
hiyo naomb nikuhakikishie kuwa usitarajie kumuona Brooklyn akisajiliwa hata
kikosi cha akiba cha Man Utd au real Madrid kama ambavyo Enzo Zidane amebebwa
na baba yake huku akiwa hajawahi kutumika mechi yeyote ya ushindani na miaka
yake 22….
***kumbe pia kuna LIKE father
UNLIKE son ****
Composed by MwanaMayeka,
instagram @mwanamayekaa
Kwa Hisani ya Official CHAX Newz
Comments
Post a Comment