Baada ya uongozi wa kundi la Yamoto Band kutoa fursa kwa kila msanii kufanya kazi zake binafsi.
msanii Aslay ameeleza mabadiliko katika maisha yake ya kimuziki.Muimbaji huyo amesema hayo kupitia XXL ya Clouds FM kwa sasa anamiss kukaa na mwenzake kwa muda mwingi kama ilivyokuwa mwanzo na hata kuonana ni kwa mara chache kwa kuwa kila mtu anakuwa bize na mambo yake.
Katika hatua nyingine Aslay ameongeza kuwa si kweli kwamba kwa sasa anatafuta mashabiki wake wapya katika muziki wake kwa sababu alishatengeneza njia nzuri akiwa Yamoto Band“Nasonga vizuri tu,
najiona kuna upya fulani lakini si wa ku-hustle wa kuwafikia tena mashabiki,” alisema "Aslay".
Source: Bongo Newz
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment