HATA "ADOLF HITLER" ANGEKUWA HAI...BASI LEO ANGEKUFA...

     HATA ADOLF HITLER ANGEKUWA HAI…BASI LEO ANGEKUFA…
Agosti 1 mwaka 1936 ulifanyika uzinduzi wa mashindano ya 11 ya michezo ya Olympic, mashindano yale yalikuwa yakifanyika mjini Berlin –Ujerumani baada ya mji ule kuushinda mji wa Barcelona - Hispania  katika kura za maoni ya kuchagua mji wenyeji wa michuano ile mapema mwaka ule… Mgeni rasmi wa mashindano yale alikuwa ADOLF HITLER ambaye kwa wakati ule alikuwa kansela na kiongozi wa kisiasa wa taifa lile maarufu kwa utengenezaji wa meli duniani, kama kawaida yake na sera zake za kina za kiongozi yule alipiga marufuku MYAHUDI yeyote kushiriki mashindano yale ila kutokana na shinikizo la mataifa mengne washiriki kama Marekani ilibidi alegeze kidogo na hapo akaruhusu wayahudi wa mataifa mengine isipokuwa waishio Ujerumani hawakuruhusiwa hata kusogea karibu na viwanja yalipofanyikia mashindano yale… .jioni ya siku ile “mbaguzi” HITLER alishuhudia maajabu ambayo hakuyatarajia… Mwanariadha MWEUSI raia wa Marekani Jesse Owens alishinda mbio za mita 100 kwa kuweka record ya dunia kwa wakati  huo ya kutumia sekunde 10.3,ndio hivyo ADOLF HITLER alishtuka sana na kutoyaamini macho yake ya kwamba imekuwaje binadamu mweusi akawazidi maarifa wazungu?  Kumbuka HITLER aliwabagua hadi wazungu wenzie (WAYAHUDI)  na siku ile aliyaona maajabu ambayo kama angejaaliwa kuwaona wajukuu zake basi nashaka angewasimulia. ….Ndugu yangu, tangu saivi ninapoandika makala hii PAUL POGBA ndiye mwanasoka ghali duniani akiwa nathamani ya karibu euro milioni 90..huyu ni Mfaransa mweusi ambaye asili yake ni Afrika Magharibi… Mchezaji bora wa ligi kuu England ni NGOLO KANTE.. .jina lake tosha linakuaminisha kuwa jamaa ni mweusi kama pua ya mbwa na hata akioga kwenye pipa la Caro light hawezi kuwa mweupe… Mfungaji bora wa ligi ya kwao Ujerumanini PIERRE -AUBAMEYANG sasa huyu ni Mwafrika haswa japo mama yake ni Mhispaniola.. .kwenye masumbwi bingwa wa uzito wa juu duniani ni ANTONY JOSHUA kijana mwenye asili ya Nigeria lakini kakuliana kuishi Uingereza…huko huko kwenye uzito wa kati bingwa wa dunia ni FLOYD MAYWEATHER .kwenye tenis ndugu wawili wa Marekani weusi SERENA na VENUS wameufanya kuwa wao….Kule kwenye mbio za magari yaendayo kasi Mwingereza mweusi LEWIS HAMILTON anawanyanyasa wazungu kila uchwao, Nchi alikozaliwa Hitler (Austria)  mwanasoka mwandamizi wa timu ya Taifa ni DAVID ALABA… Naskia jamaa alikuwa anapenda mziki sasa nadhani angeziba pamba masikioni maana huko kina Lil Wayne. Nicki Minaj. Jay Z. P-Diddy kote wamepateka (wagumu wote hupenda Hip Hop, nahisi naye alipenda Hip Hop pia) kule kwenye riadha mwanaume USAIN BOLT amenyanyasa hadi kastaafu na kuwaachia kina JUSTIN GATLIN na YOHAN BLAKE waendeleze ubabe, kumbuka hata raisi wa Marekani miezi nane iliyopita alikuwa MWEUSI pia…
**ukiniuliza kama leo ADOLF HITLER angekuwa hai basi nadhani angekuwa mahututi hospitalini akitafunwa na kiharusi kilichosababishwa na hasira na chuki dhidi ya maendeleo ya MWEUSI mbele ya MZUNGU**
Composed by MwanaMayeka, instagram@mwanamayekaa
 Kwa Hisani ya Official CHAX Newz

Comments