Leukemia ni Saratani
inayoshambulia tishu za mwili zinazohusika na utengenezaji wa damu zikiwemo
supu ya mifupa (bone marrow) na mfumo wa lymph (lyphatic system). Kwa maneno
rahisi, leukemia humaanisha saratani ya damu. Kuna aina mbalimbali za leukemia,
nyingine zikiathiri watoto na nyingine zikiathiri zaidi watu wazima.
Kwa kawaida leukemia huanzia kwenye chembe nyeupe za damu yaani white blood cells, ambapo mwili huzalisha kiwango kikubwa cha seli zenye maumbo mabaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi zake sawasawa. Kazi ya chembe nyeupe za damu ni kulinda mwili dhidi ya vimelea waletao maradhi mbalimbali.
Kinachosababisha Leukemia;
Kama zilizo kwa aina nyingi za saratani, mpaka sasa chanzo halisi cha leukemia hakijulikani. Hata hivyo, wanasayansi wanadai kuwa leukemia hutokea kutokana na mkusanyiko wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vinavyohusu sababu za kinasaba (genetic factors) na kimazingira.
Kama zilizo kwa aina nyingi za saratani, mpaka sasa chanzo halisi cha leukemia hakijulikani. Hata hivyo, wanasayansi wanadai kuwa leukemia hutokea kutokana na mkusanyiko wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vinavyohusu sababu za kinasaba (genetic factors) na kimazingira.
Kwa ujumla, leukemia hutokea pindi chembe nyeupe za damu
zinapobadilika muundo wake wa kinasaba yaani viasili vyake vya DNA, ambavyo kwa
kawaida hubeba maelekezo yanayoifanya seli yeyote ya kiumbe hai iweze kuishi,
kutenda kazi zake, kujizaa na hata kufa, vinapobadilika maumbile na muundo wake
kutokana na sababu mbalimbali. Kitendo cha kubadilika kwa maumbile na muundo wa
DNA hujulikana kama mutation. Ndiyo kusema basi, seli yeyote iliyopatwa na
tatizo hili huwa na tabia ya kukua kwa haraka na kujizaa (kujigawa) kwa kasi
zaidi kuliko kawaida, na pindi
inapofikia muda wake wa kufa seli hiyo hugoma kufa badala yake
huendelea kujizaa zaidi hatimaye kusambaa kwa wingi katika mfumo mzima wa
damu, hali inayosababisha saratani ya damu.
Vihatarishi vya Leukemia
Ndiyo vipo , Pamoja na kwamba chanzo halisi cha saratani ya damu
hakijulikani, lakini kuna mambo ambayo humuongezea mtu hatari ya kupata ugonjwa
wa saratani ya damu.
Mambo ambayo yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya
damu ni pamoja na
Historia ya matibabu ya saratani hapo kabla Watu ambao wamekuwa
kuwa na aina nyingine za saratani hapo awali, na wakati wa matibabu wakapewa
tiba ya mionzi au madawa makali ya
saratani, wapo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya damu kwa
sababu baadhi ya dawa hizi pamoja na mionzi huwa na tabia ya kuathiri pia seli
nyeupe za damu pamoja na tishu zinazotengeneza seli hizo.
1. Kuwa na magonjwa mengine ya vinasaba: Ingawa haieleweki
sawasawa uhusiano wake ulivyo, kuwa na baadhi ya magonjwa ya kinasaba kama vile
ugonjwa wa Down syndrome, yasemekana huongeza uwezekano wa muathirika kuugua
pia ugonjwa wa saratani ya damu.
2. Baadhi ya magonjwa mengine ya damu: Watu wenye magonjwa
mengine ya damu kama vile ugonjwa wa damu unaoshambulia tishu za supu ya mifupa
na kuzifanya zizalishe seli nyingi za damu bila uwiano unaotakiwa
yaanimyelodysplastic syndromes, huongeza pia uwezekano wa mtu kuugua saratani
ya damu.
3. Kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi: Watu ambao wamewahi
kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi kama vile mlipuko wa mabomu au kulipuka kwa
vinu na mitambo ya nuklea (nuclear reactors), wana hatari kubwa zaidi ya kupata
saratani ya damu pamoja na saratani nyingine.
4. Kupigwa/kutumia baadhi ya kemikali: Watu waliowahi
kukumbana na baadhi ya kemikali kama vile benzene au zile zinazotumika kwenye
viwanda vya kuyeyusha vyuma au kutengeneza
magurudumu au mabomba ya plastic, nao pia wapo katika uwezekano
mkubwa wa kupata saratani ya damu.
5. Uvutaji sigara: Jambo hili pia huongeza uwezekano wa kupata
aina mojawapo ya saratani ya damu.
Kuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia: Watu ambao,
baadhi ya ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu, nao pia wana uwezekano mkubwa
wa kupata saratani ya damu. Hata hivyo, hii haina maana kwamba leukemia inaambukizwa
isipokuwa kuna uhusiano wa kifamilia tu katika kusababisha ugonjwa huu.
Jambo moja la kufahamu ni kuwa, wapo watu wengi ambao wamewahi
kukumbana na vihatarishi nilivyovieleza hapo juu bila kupata leukemia,
kadhalika wapo waliopata leukemia bila kukumbana na kihatarishi hata kimoja
kati ya hivi.
MATIBABU YA SARATANI YA DAMU
- Matibabu
hutolewa kulingana na hatua ya ugonjwa ilipofikia.
- Kwanza
safisha damu yako,
- Zipo
dawa nyingi za asili ambazo hutibu kansa , dozi ni kulingana na aina ya
kansa na stage ilipofikia
- Mfano
Majani ya mstafeli yana uwezo wa kuziua seli za kansa aina yeyote mara
10,000 ya mionzi.
- Chukua
majani ya mstafeli yaaafishe vizuri kisha yaponde kwa Blenda kutengeza
juisi yake.
- Mgonjwa anywe nusu kikombe kutwa mara tatu siku 90.
Comments
Post a Comment