SULEIMANI MATOLA AMENIFANYA KUWA BORA - DENIS RICHARD.


                                 Golikipa wa klabu ya Simba SC, Denis Richari


Golikipa wa klabu ya Simba SC, Denis Richard amezungumzia namna anavyojiamini na uwezo mkubwa aliokuwanao katika mchezo wa soka.

     Richard ambaye ni shabiki mkubwa wa golikipa wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Porto, Iker Casillas ameyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa timu hiyo.

“Uwezo wangu nauwamini na hauwezi kuwa bora pasipo kupitia mafunzo na kuwa na mtu mwenye uwezo wa kuendeleza uwezo niliokuwa nao.      “Kwahiyo kipaji changu na uwezo wangu ni mwalimu ndiye atakaye endeleza, kuna makocha wawili sitokuja kuwasahau kwenye maisha yangu ya mpira kwa sababu wao ndio walionifanya mpaka nikawa na uwezo huu niliyokuwa nao”.      “Wakwanza sitomsahau Meja bakari yeye ndiye aliyenifanya nikatambua kipaji changu, na wapili ni Suleiman Matola alichangia mimi kuwa bora zaidi na kujulikana,” amesema mlinda lango huyo wa Simba.

Source:Bongo Newz

Designed by CHAX C

Comments