STEREO AELEZA NAMNA ALIVYOKUTANA NA "DIAMOND PLATINUMZ" NA KUPEWA NAFASI "WCB".




Rapper Stereo ameeleza namna alivyokuta na Diamond Platnumz hadi kufikia hatua ya kufanya kazi katika lebo yake ya WCB

Stereo ambaye hapo jana alitoa wimbo ‘Mpe Habari’ aliomshirikisha Rich Mavoko, amesema siku ambayo Diamond na AY wanatambulisha Zigo Remix ndipo Diamond alisema Stereo ni miongoni ya msanii anaotamani kufanaya nao kazi na habari zilipomfikia ndipo akamtafuta.

“Nikatafuta time nakumuona, nikamwabia nimekuja kuappreciate ile recognition kwa sababu sio kila mtu anamuelewa Stereo na sio kila mtu anajua thamani ya Stereo, lakini katika ukubwa wako umeona sio kitu unaweza kusema na umma kuwa unatrust talent ya Stereo.

“Akaniuliza kwanini nipo kimya, Stereo social network zimekufanya nini mbona unaweza kufanya vitu vikubwa sana kupitia mitandao ya kijamii, kwanini unapenda kujificha. Mimi nakuambia una kitu kikubwa kitoe, nataka ufanye kazi kisingizio sio studio, Laizier huyo hapo, mimi nitamonitor mambo yote. Wewe unaflow kali lakini huna chorus kali, hapa ni nyumba ya machorus makali,” amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM na kuongeza.

“Siku nimepangiwa kurekodi tunanza kutengeneza beat na Laizier, Rich akaingia na vibe ikaongezeka mule ndani na beat ilikamilika ndani ya muda mfupi, baada ya kurekodi kuna kipande katika huu wimbo nilirudishwa, Chibu alitaka hivyo.

 So unarudi unafanya, na unaona nguvu ya pamoja na kila mtu amenipokea kama brother, sijajisikia ugeni ni kama nipo tu siku nyingi Wasafi,” amesema Stereo.

Source:Bongo Newz

Designed by CHAX C

Comments