Msanii wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB, Harmonize amesema safari yake ya Miami nchini Marekani ilikuwa ni kwa ajili ya kazi na sio kupumzika, huku akitoa sababu za mpenzi wake ‘Sarah’ kujumuika nae.
Muimbaji huyo amesema si kweli kwamba alienda kutambulishwa nyumbani kwa mpenzi wake kwani walishafanya hivyo siku nyingi.
“Miami nilikuwa na project sio kupumzika, kuna vitu nilikuwa nafanya, nina project kubwa sana Mwenyenzi Mungu amebariki imeisha salama na nimerudi, nilipokuwa kule wife alikuwa na project zake,” Harmonize ameiambia XXL ya Clouds FM.
“Yeye pia alikuja kule kwa sababu sasa hivi Italy kuna baridi sana, kwa hiyo Miami ni mji kama una joto kidogo. Sio utambulisho mbona siku nyingi tushatambulishana. Halafu pia alitakiwa asafiri hapa katikati kwa sababu kitoto kikishakua kikubwa atazuiwa kupanda ndege, sasa hivi ale good time asafiri, asafiri kidogo,” ameongeza.
Source:Bongo Newz
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment