STAR "DIAMOND PLATINUMZ" AKANA KUWA HAKUMUANDIKIA "WEMA SEPETU" WIMBO "I MISS YOU"



     
Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema si kweli wimbo wake mpya ‘I Miss You’ aliuandika maalumu kwa ajili ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu.

Akizungumza na kipindi cha The Playlist cha Times FM, Diamond ameeleza yeye kuandika nyimbo kutokana na hisia alizonazo kwa wakati huo na huangali soko lipo vipi.“Hapana, sio kweli kwa sababu Wema hana mtoto, hana familia is just to me, unajua Mwenyenzi Mungu amenibariki sana kuandika nyimbo za feeling, unajua tunatafuta market na ili tukue kimuziki ni lazima na muziki mwingine tufanye ili tusi-disappoint wa nyumbani ni lazima uwape chao na kule (kimataifa) ufanye,” amesema Diamond na kuongeza.              “Huwezi kuamini ilikuja tu, nikiandika nyimbo za mahusiano kama hizi sometime chozi linanitoka, nakumbuka mara ya kwanza huu wimbo nimeuandika nipo kwenye ndege sijui nilikuwa naenda wapi, nikawa napata feeling nikiandika topic hii itakuwa vizuri na Mungu kanijalia naweza kubadilika katika muziki wa tofauti tofauti,”


Source:Bongo Newz


Designed by CHAX C

Comments