Wakati fulani mwaka 2003..ilikuwa usiku wa jumapili
fulani hivi,niliamshwa na kelele za baba yangu mzazi mzee Mayeka akipiga kelele
na yowe lisilo la kawaida..ule “mzuka” wake na yale makelele yalituzindua
usingizini mimi na kaka yangu ..katika akili yetu ya kitoto tuliamka na kabla
ya kuhoji kilichotokea tiyari alikuwa akitamka maneno fulani kwa sauti ya juu
akisema “jamani simba imeshinda..simba imeshinda misri..” sasa nikaanza kupata
picha..asubuhi ya siku ile alikuwa ametusimamia kufanya zoezi la kuchimbia
mlingotiwenye bendera yenye mistari ya rangi nyekundu na nyeupe..ambayo alikuwa
ametoka kuinunua siku chache zilizopita..baada ya wiki chache zilizofuata
alianza kutuchukua kwenye baiskeli yake na kwenda kijiji cha pili kuiangalia ile timu yake ilomfanya ajitoe “ufahamu”
usiku ule ikicheza kwenye luninga katika hatua ya robo fainali ya ligi ya
mabingwa afrika…Nimewahi kuishuhudia simba mara kadhaa lakini sijawahi kuiona
simba yenye mseto mzuri wa wachezaji ndani ya uwanja kama ile,kazi nzuri
iliyokuwa ikifanywa na simba ile iliifanya iaminike sana kwa mashabiki wake akina
Mzee Mayeka,hakika mzee wangu ni shabiki wa simba haswa..ile simba
ilimuaminisha ushindi hata kabla haijakanyaga taifa kucheza na mwarabu au
sheikh amri abeid kucheza na AFC au palsons ya askofu Mollel,Kambarage kucheza
na Kahama united,Sokoine kucheza na Tukuyu au prisons..kote ambako simba ile
ingetia mguu tayari Mzee wangu Mayeka alishaamini isingemuacha mtu salama na
hili lilizidi kuiboresha desturi yake ya kutupelekesha kuchimbia ile Bendera
yake yenye rangi nyeupe na nyekundu nje ya nyumba yetu kila siku asubuhi ambayo
jioni yake simba ingecheza…Simba ile achilia mbali kuwatoa “kibahati” zamalek
iliweza kuwaduwaza 2-1 enyimba ya Daniel Okpara,Onyekachi okonkwo na kipa wao
Vincent Enyeama mbele ya Mzee Fredrick Sumaye na mamia ya wale waimba “kidedea”
walioongozwa na Mzee MagomaMoto pale shamba la bibi,..Nakumbuka vizuri pia kuwa
hulka ya ushindi ilizaa imani kubwa ya
mashabiki kwa timu hii yenye makao makuu pale kariakoo,hali iliyojenga ujasiri
na ari kwa wachezaji..unalikumbuka lile tukio la juma kaseja kudaka ile penalti
ya Numba Mumamba wa Zanaco FC(kwa sasa ndiye kocha mkuu) ya
Zambia mwaka 2004? Mashabiki walikuwa wakiimba jina la Juma muda ambao penalti
ile ya mwisho ilikuwa ikienda kupigwa,juma naye aliwajibu kiitikio kwa kupangua
penalty ile....
Leo najaribu kutathimini nagundua kuwa simba ile
ilikuwa na mseto wa wachezaji wenye vipaji haswa ,na wote walikuwa ni wazalendo
wa hapahapa nchini,simba ile iliyokuwa ikiwatoa jasho waarabu na timu za afrika
ya magharibiilikuwa pia na kocha kutoka nchi jirani tu hapa Kenya hayati mzee
Siang’a..usajili wa Okwi juzi umefanya nianze kujiuliza ni nani aliyewasajili viungo
mahiri akina Jumanne shengo Tondola na Primus kasonzo wakati ule? Ni nani
aliyekuwa anawascout akina Said Sued,Victor Costa,Christopher Alex,Steven
Mapunda,Emmanuel Gabriel,Athumani Machupa,Clement Kahabuka na Lubigisa Madata,
Simba ile iliweza kumbembeleza Joseph Kaniki lakini pale iliposhindikana
kumsajili haikupungukiwa kitu na iliendelea kufanya vizuri siku zote..nikiwa
nawaza nakumbuka pia kuwa simba ile kwa wakati ule haikuwa na afisa habari..haikuwa
na mtu mwenye kutengeneza tambo nyingi zisizo na mantiki mbele ya vipaza sauti
vya waandishi wa habari kama ilivyo sasa..jioni ya kuamkia mechi na Enyimba
ungemsikia Kassim Dewji akiongea redioni kuelezea maandalizi ya timu yake
kuelekea mchezo ule..katibu mkuu huyo angemalizia kuwaalika mashabiki wa timu
yake wafike kwa wingi uwanjani kuwaunga mkono na kweli akina mzee mayeka
wangetabasamu baada ya mchezo wa kesho yake licha ya kuwa waliusikiliza redioni.nagundua
zaidi ya kuwa kifuani mwa jezi za simba ile palikuwa na maandishi kama K.K
sukari,MeTL,na Safi unga wa ngano najiaminisha kuwa Mfanyabiashara Mohamed
Dewji alisimama vyema nyuma ya timu ile ambayo ilishuhudia mafanikio makubwa
pengine tangu tuingie karne ya 21…………..katika harakati za kumfanyia tohara
mnyama chui kunahitajika mambo makuu mawili muhimu sana..Mosi panahitajika watu
jasiri wa kumlaza chali chui mwenyewe,na hawa watu hawahitaji kuwa na nguvu tu
bali pia akili na mbinu nyingi sana,Pili anahitajika NGARIBA,huyu yeye
anatakiwa aweze kujitoa kushika kisu na kukiamuru kifanye kazi yake basi..pale
simba kwa miaka mingi tangu Mohamed Dewji asitishe ufadhili wake pametokea
kipindi cha mpito kilichoshuhudia kupotea kwa ile simba iliyowafanya akina Mzee
mayeka na rafiki yake Mzee Yahewa wachimbie bendera za timu yao nje ya nyumba
zao….Leo simba imewaajiri akina Ezekiel Kamwaga kama maafisa habari na kuenda
Congo DRC kuwachukua Linno Musombo na Kanu Mbiyavanga,haitoshi Simba hii
inaenda Mali kumchukua Komambil Keitahapa unategemea Mzee Mayeka ataitoa bendera
yake na kuichimbia? Hapana,Mzee huyu hana uwezo wa kujiamini kiasi hicho tena
maana Simba yake kabla haijaenda kuikabili DC Motema Pembe haina uhakika wa
kuondoka na pointi 4 kati ya sita za kanda ya ziwa ambazo wanazo Toto Africa na
Kagera sugar licha ya kuwainayeFeliX Sunzu wa Zambia,baada ya hapo Simba
inaamua kumbadili dereva mahiri aliyenyimwa ushirikiano na “wenye” gari lao
Mzee Rage na kumpa usukani Evans Aveva kutoka kundi la “wenye” simba, wanachama
wanamwamini kupita kiasi na kuamini kuwa huyu ndiye NGARIBA ambaye angalau
ataweza kufanikisha tohara ya chui iliyowashinda wengi,Aveva anaingia na timu
ya mangariba wenzake kutoka Friends of Simba ili wamsaidie kumlaza chali chui..anaajiri
makocha watatu ndani ya miaka mitatu..anashirikiana na kamati yake ya usajili
inayofanya kazi “ya usajili” hadi pasipo na usajili lakini wote wanaishia
kuraruriwa na chui huyo huku timu haipandi ndege kwa misimu takribani minne.huku
nje anambadili Kamwaga na kumpa shabiki damu Haji Manara uafisa habari,Huyu yeye
anajitahidi kuwaaminisha mashabiki kile kisicho halisi na kuwaahidi ubingwa
kila msimu pasipo hata kuwasiliana na makocha wake ambao ndio wanajua
kuutengeneza uhakika wa ubingwa uwanjani na siyo mdomoni…..Nagundua kuwa kwa
kizazi cha sasa Mo dewji ndiye ngariba pekee anayeweza kuiwezesha tohara ya
chui iliyoshindikana pale Simba Sc,Dewji alikuwa ngariba mkuu kipindi kile
akina Kassim dewji wakimsaidia kumlaza chali chui na hivyo aliwasaidia kumaliza
kazi ile..Dewji aliweza kushirikiana vizuri na “kamati ya usajili” ya wakati huo
na kuwapata wachezaji wenye uwezo tena hapa hapa nchini,naamini dewji
anawakumbuka vizuri watu aliofanya nao kazi wakati ulekiasi kwamba anaweza
kuwatumia hata leo maana hawa waliopo sasa hawaijui vizuri kazi yao kiasi cha
kushindwa kuvumbua wachezaji na kumfanyia usajili mchezaji mmoja mara tatu
ndani ya misimu 8,na haikushangaza ujio wa Dewji umeleta ubingwa wa FA kwa
simba na nafasi ya pili msimu uliopita ambapo kidogo Simba imezidiwa tofauti ya
magoli na bingwa, Dewji akipewa timu hahitaji sana kuwa na wahamasishaji kama Haji manara,yeye anaamini
zaidi katika kufanya uwekezaji wa moja kwa moja katika miundombinu ya soka la
kileo kama kufanya usajili madhubuti na kuandaa timu imara ya vijana kwa kizazi
kijacho(ameyaongelea haya kwenye mpango mkakati wake)anaweza kukusanya watendaji makini wa kumsaidia
kuifikisha juu simba,bahati nyingine MoDewji ni “Money in the bank” kiasi
kwamba pale hana shida kusajili wachezaji bora na mahiri hata kwa gharama kubwa,..ni
kama hivi leo tunavyosikia amewaleta Niyonzima na Okwi na bado atawalipa
mshahara wao na hata wale wengine atawalipa posho msimu mzima,..leo hata wale
wanaopinga mchakato wa yeye kupewa timu wanashangilia msaada anaoutoa wakati
huu wa usajili na kusahau ya kuwa wanapaswa kumkabidhi rasmi kisu amalize rasmi
kazi ya kumfanyia tohara huyu chui aliyewashinda…
Imeandaliwa na MWANAMAYEKA
Kwa Hisani ya #Official Toshi Newz
Comments
Post a Comment