"ROMA MKATOLIKI" AWEKA WAZI KUWA SERIKALI HAIKUMPA MSAADA WOWOTE "ALIPOTEKWA".


 
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki amefunguka na kusema kuwa ingawaje Serikali ilimsaidia mpaka kupatikana kwake kipindi alipotekwa  lakini haikumsaidia chochote mpaka kupona kwake.

Roma Mkatoliki akiwaonesha majeraha waandishi wa habari siku chache baada ya kuachiwa na watekaji .
Roma na wenzake wanne ambao walitekwa na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwaka huu na kupata majeraha makubwa kwenye mwili wake amekiri wazi kuwa Serikali haikumsaidia chochote mpaka anapona zaidi ya ndugu, Jamaa,marafiki na familia yake.

“Lahashaa! Hapana juu kwa juu tuu polisi, polisi Mwananyamala PF3 sijui nini ile, baada ya pale nikajiongoza mimi mwenyewe na familia yangu,so ikawa hivyo tuu“amesema Roma.

Hata hivyo Roma amesema ameshawasamehe na amewasahau wote waliohusika na kutekwa kwake ila amewaweka wazi tuu Watanzania kuwa hakusaidiwa chochote na Serikali katika kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kutekwa.
  “Yaliyopita yamepita tunasamehe,tunasahau waliohusika Mungu atawahukumu na mkono wake na Mungu atupe neema uvumilivu na neema ya kuwasamehe…Lakini usidanganyike na mtu anakwambia sijui alikuja akatoa bugana lake au sijui akatoa hela ya panadol, Lahashaa!“amesema Roma kwenye mahojiano yake na Times FM.


Imeletwa kwenu kwa hisani ya #Official Toshi Newz

Designed by CHAX C


Comments