NDOTO YA "RAYVANNY" KWA "JASON DERULO" YATIMIA.

 Moja ya Sifa za Members wa WCB ni kuchangamkia Fursa,panapo tokea Chance au upenyo wa kitu fulani huwa wanakishughulikia Mapema na kwa Umakini wa hali ya juu,hiyo ndio sifa ya WCB-Wasafi.
Mmoja kati ya WCB members ambaye siku chache zilizopita alinyakuwa tuzo ya BET,"RAYVANNY" amefanikiwa kukamilisha ndoto yake ya siku nyingi kabla ya kuingia WCB, aliyokuwa akitamani siku moja kuja kufanya kazi na Jason Derulo.
Hatimaye ameikamilisha leo kwa hiyo tutegemee mazuri kutoka kwa "RAYVANNY" pamoja na "JASON DERULO".

Kupitia mtandao wa Instagram, Ray ameweka picha akiwa syudio na msanii huyo na kuandika, “God bless you my brother @jasonderulo its amaizing opportunity,am so grateful for that……… Toka Saa 8 Usiku amekaa na mimi hadi Asubui…"

"Harmonize naye amepost kwenye akaunti yake ya instagram hivi..."HIVI NDIVYO TUNAFANYAGA.......!!!!KUACHA TOBO MWIKO"
Ikiwa ni ishara kuwa nafasi inapojitokeza usiipuuzie tu ukijua kuwa siku nyingine itakuja,ukifanya hivyo ujue unapishana na Maendeleo.Kumbuka Maendeleo huletwa na Kujaribu na Kujiamini.

"Diamond Platinumz pia amepost hivi..."Na venye hatufanyagi mzaha kwenye 18 zetu.........@Rayvanny &@Jason delulo,when i say #Wcb Wasafi for life I mean it Bro!!


 Kwahiyo Tutegemee vitu vizuri kutoka kwa "RAYVANNY" akiwa na "JAYSON DERULO" kwa wimbo unaokuja.

Designed by CHAX C

Comments