MWANZA: FAMILIA YANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA JIWE.



Familia moja ya watu wanne wakiwemo watoto wawili imenusurika kupoteza maisha, baada ya kuporomokewa na Jiwe kubwa kutoka mlimani, lililobomoa ukuta na kisha kuingia sebuleni katika eneo la kata ya Kishili wilayani Nyamagana mkoani Mwanza. 

Si rahisi kuamini lakini ndivyo ilivyokuwa, wakati Jiwe hilo likiporomoka kutoka mlimani majira ya jioni, watoto wawili wa familia hiyo walipokuwa wakioga nje ya nyumba, ambapo walishuhudia Jiwe hilo likiporomoka na hatimaye kukimbia huku jiwe hilo likiwafuata. 
Wakati wakiwa kwenye harakati za kunusuru maisha yao, watoto hao walioachwa nyumbani na wazazi wao ambao muda huo walikuwa kazini, walijikuta wakiponea chupuchupu baada ya jiwe hilo kugonga ukuta wa nyumba yao na kisha kugota sebuleni. 

Kisha viongozi wa mtaa huo wakazungumzia tukio hilo, huku wakiishauri jamii hususani wapiga mawe kuacha tabia ya kuchokonoa mihimili ya mawe yaliyopo mlimani, kwa kuwa wanaweza kusababisha athari kubwa vikiwemo vifo. 

Kutokana na ajali hiyo mtendaji wa kata ya Kishili Sayenda Mvanga, amewashauri Wananchi kuepuka ujenzi holela, ili kuendana na sheria za mipango miji ambazo zitawaepusha na majanga kama hayo. 

Jeshi la Polisi la Polisi mkoa wa Mwanza limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambalo halijamjeruhi mtu yeyeyote, ingawa kumekuwepo na uharibifu wa baadhi ya mali zilizokuwepo ndani ya nyumba hiyo.

Source:Muungwana

Designed by CHAX C

Comments