MWANAMUZIKI anayetamba na Ngoma ya Wasikudanganye, Faustina Charles`Nandy’ amefunguka kuwa hapendi kufanya kolabo na msanii yeyote kwa sasa bali ataendelea kukomaa mwenyewe kwenye muziki kwani anajikubali.
Akibonga na Mikito Nusunusu, mwanamuziki huyo alisema ana uwezo wa kusimama mwenyewe hivyo anaona akifanya kolabo ataonekana anabebwa kitu ambacho hakitaki kusikia ndiyo maana anaamua kukomaa kivyake.
“Najikubali mwenyewe kwa uwezo nilionao, kikubwa nitaendelea kupambana kuhakikisha siharibu ubora wa uimbaji wangu kwa mashabiki, sipendi kufanya kolabo kwani nahisi bado nina nafasi ya kusimama peke yangu na nikafanya poa,” alisema.
Source:Raha za Walimwengu
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment