
Msanii wa Bongo Fleva, AT amesema ugomvi wa Diamond na Alikiba ulianzia nchini Oman ambapo walienda kufanya show.
Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, muimaji huyo maarufu wa muziki wa mduara, amesema mashabiki wengi hawajui mwanzo wa mvutano wa wawili hao ila wao wenyewe ndio wanajua ukweli huo.
“Tulikuwepo tupo Oman kwenye hotel moja inaitwa Dream tulikuwa tuna show, kwa hiyo walikuwa wanacheza game, Alikiba amechagua Real Madrid na Diamond Barcelona, mimi nimekaa pembeni naangali watu wanacheza game yao. Ali akawa amefungwa mbili, akawa anataka kupiga free kiki kwenye game Diamond akamsukuma akamwambia halafu mwanangu nakutafuta siku nyingi,” amesema AT.
“Alikiba akanyanyuka ikabidi na mimi ninyanyuke sasa, nikamuuliza Ali tatizo nini mbona kama mnataka kupigana halafu tupo ugenini wazee vipi? Akaniambia huyo dogo kuna vitu anavifanya mimi sijavipenda,” ameongeza.
“Mwisho wa siku naona kama vile vitu vinaendelea halafu watu wanakurupuka wala tatizo wao hawalijui. Ebu watafute ukweli ulipo, sijui huyo kamtoa kwenye wimbo huyo, kuna jambo lingine ambalo lipo. Kiukweli kuna vitu ambavyo pengine wao wenyewe wanavijua ni vikubwa zaidi,” amesisitiza.
AT ameongeza baada ya Alikiba kusimama kama yeye asingekuwepo mmoja kati yao (Aikiba na Diamond) angekuwa hana meno au sikio, yaani wangepasuana.
source:Bongo Newz
DESIGNED BY CHAX C
Comments
Post a Comment