MREMBO "GIGY MONEY ASEMA "SIO LAZIMA WOTE TUIMBE".


Mrembo "Gigy Money"

Video Vixen, Gigy Money amesema si lazima kwa warembo wanaofanya kazi kama yake kuingia katika muziki, huku akiweka bayana sababu za yeye kuingia katika tasnia hiyo.

Gigy Money amedai yupo serious na muziki na sababu yeye kufanya hivyo ni kutokana na watu kumchukulia poa katika kazi yake ya awali.
“Ni kweli si lazima wote tuimbe lakini kibongo bongo ukifanya vile sana unakuwa huwezi kufanya na mambo mengine, yaani hutoboi. Watu wanakuona wewe miyeyusho, yaani wewe huna akili kwa sababu watu wanachukulia Gigy ni mtu kalanduka, kapinda kumbe mimi niliangalia hela, halafu niliangalia na mkwanja,”
amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Nipo serious na leo naenda kufuata video yangu, kwa hiyo ikiisha Ramadhan, nasubiri wamalize kufunga nianze balaa langu. Ngoma inaitwa Papa, kuna kijana anaitwa Marioo ndiye aliyeandika na ndiye nimemshirikisha kwa sababu ni mwandishi mzuri pia,” amesistiza Mrembo "Gigy Money"

Source:Bongo Newz

Designed by CHAX C

Comments