Msanii wa Bongo Fleva, Jux amesema haikuwa kazi rahisi hadi yeye kumaliza masomo yake ya elimu ya juu nchini China.
Muimbaji huyo amesema kuwa katika miaka mitano aliyosoma kuna wakati alikuwa anakosa mitihani kwa sababu ya show lakini anaishukuru familia yake kwa kuwa karibu na yeye.
“It’s not easy at all lakini nashukuru sana rafiki zangu ambao wamenizunguka, familia yangu ni watu ambao walikuwa wananipa sana moyo, walinieleza kila kitu kinawezekana usikate tamaa, naweza nikamaliza nikafanya vitu vyote, naweza nikafanya biashara, muziki na kusoma pia,” Jux ameiambia XXL ya Clouds FM.
“Namshukuru Mungu nimemaliza leo, so kila kitu kinawezekana naweza nikakuambia muda wako tu unavyoupanga na changamoto zipo nyingi, kushindwa sio tatizo ila hutakiwa kuacha. Kuna mitihani kama miwili hivi nakumbuka nilikuwa nipo Bongo nina show wenzangu wakafanya lakini nilikuja nikarudia,
so changamoto kama hizo zinapatikana na inabidi vitu vyote viende kwa wakati mmoja lakini muda wako ni kitu ambacho kinaweza kukufanya ukawa sawa, namshukuru Mungu nimemaliza kwa hiyo sasa hivi ni muziki biashara,” aliongea Jux.
Source:Bongo Newz
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment