WIKI hii imekuwa gumzo katika ukurasa wetu wa Facebook baada ya mashabiki wa Wema na Sanchi kutambiana kila mmoja kuwa ataibuka mshindi.
Kama tujuavyo tupo na washiriki wanne tu ambao wataelekea katika fainali itakayofanyika Sikukuu ya Idd ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem.
Unavyodhani nani kati ya hao washiriki yaani Sasha, Wema, Masogange na Sanchoka ataibuka mshindi? Jibu ni rahisi, chukua simu yako, nenda kwenye sehemu ya kuandikia SMS kisha andika SHEPU acha nafasi ,andika namba ya mshiriki unayemtaka abaki na utume kwenda 15542. Namba zao ni Wema ni 18, Sanchi – 25, Sasha -12 na Masogange -23.
Hii ni kwa wateja wa VODACOM pekee.
Comments
Post a Comment