KIPI BORA BAINA YA "UTU" AU "MALI"??


Tuanze kwa kujiuliza tena je kipi ni bora kati ya utu na mali? Maana binafsi huwa sielewi hasa pale wanasema utu ni bora kuliko mali, huwa sielewi kwa sababu kauli hiyo ipo sawa kabisa lakini haina ukweli katika jamii hii, unajua ni kwanini, tulia nikujuze vizuri. Jamii ya leo inathamini mali kuliko utu wa mtu. Pesa na mali nyinginezo zimepewa kiupambele kuliko kitu kingine katika sayari hii. 

Pia ule usemi wa kusema mahitaji muhimu kwa binadamu ni chakula, malazi na mavazi umegeuka na kusema mahitaji ya binadamu ni pesa kwanza hayo mengine yanapatikana kwa uwepo wa pesa kwanza, wapo wanasema pesa sabuni ya roho, wapo vijana pia wanaosema ya kwamba pesa madafu na majina mengineyo mengi. Ukichunguza kwa umakini juu ya hiyo pesa ndiyo ambayo inatengeza Mali. Mali hizo ni kama nyumba, viwanja, magari ni vitu vinginevyo vingi ndizo zinazougeuza thamani ya utu. 

Hebu tuendele kujiuliza na kutafakari juu ya kauli hiyo. Je ni watu wangapi ambao huwatumia vijana na wasio vijana katika masuala mazima ya usambaji wa madawa ya kulevya, ujambazi, kumiliki madangulo? bila shaka idadi ya watu hao ni wengi mno. Pia ukiendelea kufanya uchunguzi huo huo utagundua ya kwamba wamiliki wa watu hao wao hujali mali zaidi kuliko utu. 

Tusonge mbele na kuangalia kusuhusu wale wanaofanya kazi ya kulinda mali za watu wengine (walinzi) ukichunguza mishahara yao na Mali ambazo wanazilinda ni tofauti. Mali hizo sina thamani zaidi ya utu wa mtu hii ni kutoka na wajiri wanavyoona, hapo ndipo panaponifanya ni kubalie na yule aliyesema pesa mbele kuliko utu. Sijui tunaelekea wapi katika dunia ya leo? maana hatuthamianiani hata kidogo 

Bila kutoka nje ya mada ya leo ni kwamba binadamu katika maisha ya kawaida hatuthamini hata chembe maisha ya mtu mwingine hata chembe. Huenda ukawa hajanielewa ila ukweli ni kwamba hebu jaribu kufanya uchunguzi wa watu  ambao wanaendesha magari ya abiria na mizigo, pindi wapatapo ajali mara kadhaa wamiliki Wa magari hayo utawasikia wanaulizia muonekana wa gari kuliko vifo na majeruhi ambayo yametokea. Kwa mfano huo ndipo utakapogundua ya kwamba mali ina umuhimu kuliko utu wa mtu mwingine. 

Basi kama ndivyo hivo tuweze kubadili mtazamo badala ya kusema mali ni bora kuliko utu na iwe utu ni bora kuliko mali kwa kuthamini utu na kazi ambayo anaifanya mtu, kufanya hivi kutasaidia kila mtu aweze kufanya kitu kwa upendo na si kwa hofu. Pia endapo Utajali utu utasabisha utendaji wa kazi uongezeke mara dufu zaidi. Hata hivyo ikubukwe ya kwamba Utu haununuliwi hivyo ni vyema kujali utu wako na mtu mwingine ili kuongeza ufanisi wa mafanikio.


Source:Muungwana


Designed by CHAX C

Comments