HATIMAYE "RAYVANNY" AIBUKA SHUJAA KWENYE TUZO YA "BET".





Hatimaye kwa mara ya kwanza Tanzania imefanikiwa kunyakua tuzo ya BET.
Tuzo hizo ambazo zimegaiwa usiku huu mjini Los Angeles, katika ukumbi wa Microsoft Theater Centre, Rayvanny ambaye alikuwa akiwania tuzo hizo kupitia kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act amefanikiwa kuibuka kidedea.

Wasanii wengine ambao alikuwa akishindana nao katika kipengele hicho ni Dave (Uingereza), Amanda Black (Afrika Kusini), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na Skip Marley (Jamica).




Baada ya kushinda tuzo hiyo, "Rayvanny" kupitia mtandao wake wa Instagram ameshukuru kwa kuandika,                 “God is good all the time.Asante Mungu wangu Ulieniumba,Unaejua mwanzo na mwisho wangu.Uliyaona machozi yangu nilipokua mpweke sina furaha na mwenye majonzi mengi.WEWE NDIYE MUWEZA…”                “Asanteni wadau Wote mlio VOTE kwa Ajili yangu Ushindi umerudi Nyumbani. SITOACHA KUSHUKURU UONGOZI MZIMA #WCB @babutale @sallam_sk @Diamondplatnumz @mkubwafellatmk @kameboy_j @ricardomomo thanks Alot @bet_intl @betawards @bet_africa #WCBFORLIFE MAMA I LOVE YOU,” ameongeza         "Rayvanny"


Source:Bongo Newz


Designed by CHAX C

Comments