HARUNA NIYONZIMA:INUNULIE BETRI JIPYA HIYO SAA YAKO
Moja ya nguzo na
kanuni sahihi katika njia ya kufikia
mafanikio ya hapa duniani ni matumizi sahihi ya MUDA, imekuwasuala la kawaida
kwa vijana wengi wa kileo wakitumia saa kama mapambo tu ya kuongezea muonekano
wa nyumba au labda mwili (saa za mkononi) japo kiuhalisia kazi ya saa ni
kumuonyesha MUDA yule mtumiaji wake ….muda wowote kuanzia hivi sasa Haruna
niyonzima anatangazwa kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kukipiga kwenye ligi ya
mpira wa miguu hapa Tanzania …Ndiyo ni kweli anasaini mkataba wa miaka miwili Simba
SC kwa dau la takribani millioni 150 huku ikisemekana pia akipewa nyumba ya
kuishi na watoto wake wakisomeshwa bure… Niyonzima amekuwa mwerevu sana… na
amekuwa mwerevu hata kuliko wengi wetu ambao leo tunamtukana na kuchoma jezi
yake eti kisa amehamia timu ya watani wetu wa jadi na kusababisha kejeli nyingi
kutoka upande pili wa mitaa ya kariakoo….Uamuzi wa Niyonzima umekuja wakati
sahihi kabisa,ni wakati sahihi kwake na kwa wanasoka na wapenzi wa soka la
Tanzania ,ni wakati ambao Wachezaji na wadau wa soka tulikuwa tunajiuliza maana
halisi ya neno PROFESSIONALISM kwenye soka la kileo…. Haruna anazidi kutufungua
kuwa zaidi ya burudani soka ni mchezo wa kulipwa kwa dunia ya leo..na ili
ukulipe ni sharti uitumie vizuri saa iliyopo mkononi mwako….ukumbuke vizuri MUDA
ulionao kabla haujageuka kuwa historia, Mwanasaikolojia Abraham Muslow aliwahi kusema
“mtu pekee ambaye unapaswa kupambana kumzidi ni yule uliyekuwa jana “ ..Haruna
amesanuka na kuitizama zaidi saa yake,baada ya hapo akageuza shingo na
kumuangalia Haruna Akizimana Niyonzima mwenyemiaka minane pale gisenyi-Rwanda,akagundua
kuwa Haruna yule bado anamdai maisha mazuri zaidi aliyoishi kuyaota yatakuja
kupitia miguu yake ,…Niyonzima siyo Nadir Cannavaro ambaye huenda tangu anakua alikuwa
na ndoto za kuchezea Yanga na Simba,Haruna yeye amekua na ndoto ya kutengeneza
pesa kwa kuchezea Simba, Yanga na zinginezo ziitwazo klabu za soka ….Asante
HARUNA NIYONZIMA ,sasa unaweza kuipa zawadi ya betri jipya hiyo saa yako ya
mkononi kwa kukupa thamani sahihi kwa wakati sahihi ..THIS IS FOOTBALL
By MwanaMayeka
Written by MWANAMAYEKA
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment