Muigizaji wa filamu nchini, Gabo Zigamba amefunguka na kusema hana uhusiano wa kimapenzi na muigizaji mwenzie Wema Sepetu zaidi ya wao kufanya kazi pamoja
Gabo amelazimika kusema hayo mara baada ya kuenea tetesi kuhusu jambo hilo wakati akitengeneza filamu yake mpya ya Kisogo, kitu ambacho ameweka bayana kuwa si kweli.
“Mimi na Wema ni kazi tu. Hakuna kitu cha tofauti ambacho tulikifanya au tulikianzisha tukiwa location kwa sababu mpenzi wake alikuwa anakuja nae mara zote ambazo tulikuwa tuna-shoot,” Gabo ameiambia FNL ya EATV.

Aliendelea kwa kusema, “Kipande vyote alikuwa na sisi bega kwa bega sasa hata kama ni hayo mahusiano tungeyaanzisha muda gani? Watu wasifikiri tofauti kwani ukaribu wangu na Wema Sepetu umezalisha filamu ya Kisogo ambayo tunaamini watanzania wataifurahia”.
Source:Bongo Newz
Designed by CHAX C
Source:Bongo Newz
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment