FIGISU ZA TADY ETEKIAMA
NA MAFANIKIO YA VIJANA KUTOKA CONGO
Mwanzoni mwa wiki hii ilichezwa
mechi ya kundi A hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika ikizishirikisha As
Vita ya Congo DRC na St George ya Ethiopia, As Vita walishinda kwa magoli mawili
dhidi ya moja la St George, kilichonivutia sio mchezo wenyewe bali yule
mfungaji wa magoli yote mawili ya As Vita aitwaye TADY ETEKIAMA ,unalikumbuka vizuri lile sakata
la timu ya taifa ya Rwanda kuondolewa kwenye hatua ya makundi ya kufuzu michuano
ya mataifa ya Afrika mwaka 2015 nchini Guinea ya ikweta lililotokea agosti mwaka
2014??sasa huyu ndiye alikuwa muhusika mkuu…Wakati wa mechi za mchujo baada ya
Libya kutolewa na Rwanda walienda kukata rufaa CAF ya kwamba yule Mrwanda aliyewapiga
hatrick anayeitwa DADDY BIRORI utambulisho waushiriki wake kwenye michuano ya ligi
ya mabingwa Afrika mwaka 2009 ulionyesha kuwa ni raia wa Congo DRC, lakini katibu
Mkuu wa Ferwafa (shirikisho la soka nchini Rwanda) Olivier Mulindahabi alijibu tuhuma
hizo kuwa ni kweli lakini hazina mashiko kwa maana tiyari Daddy Birorini raia halali
wa Rwanda baada ya kuishi nchini humo kwa miaka mitano.. CAF ikatupilia mbali pingamizi
la Libya,hatua iliyofuata Rwanda walifanikiwa kuwatoa Congo Brazzaville ambao nao
hawakukubali wakaamua kupeleka rufaa CAF kwa kuhoji uhalali waDady Birori… CAF
walipitia malalamiko yale na kutangaza kuiondoa mashindanoni Rwanda tarehe18
agosti 2014,kwa maelezo yao CAF walidai kuwa mchezaji wa Rwanda aitwaye Dady Bilori
alikuwa na utata kwenye uhalali wa uraia wake, walisema alimiliki pasipo timbili
zenye taarifa tofauti,pasipoti moja yaRwanda ilionyesha kuwa Dady Bilori amezaliwa
12/12/1986 na nyingine ilikuwa ya Congo DRC iliyoonyesha kuwa na jina Tady
AgilEtekiamana ikiwa na tarehe ya kuzaliwa 13/12/1990….kutokana na mkanganyiko ule
Rwanda walitolewa na nafasi yao wakapewa Congo Brazzaville hukupia Dady Bilori akifungiwa
miaka miwili kucheza soka…imethibika kuwa jina halisi la “Dady Bilori” ambaye kiasili
alizaliwa Congo DRC ni Tady AgilEtekiama,wakati unajiuliza ya kwamba alilitoa wapi
jina la Dady Bilori naomba nikurejeshe nyuma miaka takribani Kumi hivi… Yanga
walifanikisha usajili wa mbwe mbwe nyingi wa mchezaji kutoka APR ya Rwanda marehemu
Raulent Kabanda (alifariki 2010) hiyo ikiwa ni mwaka 2007,Kabanda kiuhalisia alikuwa
ni raia wa Congo DRC, alipotua Yanga ajabu ilikuwa ni kwamba alilikana jina la
Raulent Kabanda na kuwaomba watanzania wamwite jina lake halisi ambalo ni Mukandila
Tshitenge-Pierre, alipoulizwa ni kwa nini alidai kuwa jina la Raulent Kabanda alikuwa
akilitumia kufanyia “kazi” nchini Rwanda basi na hivyo sasa (wakati huo) angependa
ajulikane kwa jina lake halisi lakini kwa vile wabongo ni wabishi waliendelea kumwita
jina walilolizoea la Kabanda,ukiwa bado unafikiria nini kilichosababisha haya majina
yake mawili nikukumbushe kuhusu MbuyuTwite, ndiyo huyu huyu Mbuyu Twite aliyetoka
kukipiga Yanga mwaka mmoja uliopita,huyu asili yake nimzaliwa wa Congo DRC lakini alipata kuitumikia timu ya taifa ya
Rwanda kwa ngazi ya kimataifa lakini akitumia jina la ERIC GASSANA Kama
unabisha rejea mashindano ya cecaffa chalenji hata ya mwaka 2011 yaliyofanyika Tanzania,Twite
alitumia jina Eric Gassana kwa ngazi ya kimataifa akiichezea Rwanda lakini akiwa
APR na Yanga anatumiajina lake halisi la Mbuyutwite…ukiwa bado unafikiria kuhusuTwitesiovibayanikakumbusha
pia kuhusu nahodha wazamani wa Rwanda marehemu Mutesa Mafisango.. huyu naye alikuwa
ni raia wakuzaliwa wa Congo DRC lakini alikuwa akiiwakilisha Rwanda kwa ngazi ya
kimataifa kwa jina la Mutesa Mafisango… lakini aliposajiliwa na Azam FC ya
Tanzania alianza kutumia jina la Patrick Mafisango,aliwahi kukaririwa akisema kuwa
jina la Mutesa amelipata Rwanda na kwamba hali kuwa jina lake halisi, na bado aliyewahi
kuwa dereva na swahiba wa karibu wa Mafisango aliwahi kukaririwa akisema kuwa Mafisangoaliwahikumwambiakuwajina
lake halisini Patrice Mafisango na siyo Patrick,………..kufikia hapa nagundua kuwa vijana Wacongoni watafutaji sana,na katika utafutaji wao hujikuta wakivuka
mipaka na kuibukia nchi za jirani zikiwemoRwanda,BurundinaTanzania,wakifikahapahuamuakutengenezahatizakusafiria(pasipoti)
mpya za nchi waliyofikia maana yake ni kwamba sasa wanakuwa wanamiliki pasipoti
za nchi mbili tofauti, unalikumbuka sakata la Shaban Nonda kuondoka Yanga
nakujiunganaVaal Proffesionals ya Afrika Kusini mwaka 1994? Ilikuwa hivi,viongozi
wa Yanga walizuia hati yake ya kusafiria ya hapa Bongo kwa kushinikiza asiondoke,
kumbe jamaa alikuwa na hati nyingine ya kusafiria ya kule Burundi hivyo akatoroka
na kutimkia Afrika kusini….wanasoka wengi kutoka nchi ya DRC wanaotafuta njia za
kutoka kupitia nchi za jirani wamekuwa wajanja sana kuitumia mbinu hii nanaona wengi
imewasaidia sana kufanikiwa kimaisha..
Dady Bilori (Tady Etekiama) wa kwanza kushoto waliosimama akiiwakilisha timu ya Taifa ya Rwanda, wa pili kushoto walioinama ni Eric Gassana (Mbuyu Twite). |
Written by MWANAMAYEKA
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment