UTANGULIZI
Mti wa Mlonge una faida nyingi ambazo hazifahamiki kwa watu wengi. Faida za mti huu
zinatokana na sehemu mbalimbali za mti huu ambazo ni maua, majani, magome na matunda
na zina faida nyingi kwa afya ya binadamu.
Maua ya mlonge huzalishwa hata kipindi ambacho hakuna mvua. Mti huu una viinilishe
ambavyo huweza kutumika kuboresha afya ya watoto wakati wa njaa.
Majani ya mti huu yanastawi hata kipindi cha ukame ambapo ukuaji wa mazao ya chakula ni mdogo. Majani haya yana kiwango kikubwa cha vitamin B na C.
Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimeonyesha kuwa Mlonge una faida zifuatazo:
- Unaongeza kinga ya mwili
- Majimaji ya majani hutumika kama dawa ya ngozi
- Majimaji ya majani hurekebisha msukumo wa damu
- Unapunguza maumivu ya kichwa
- Majimaji ya majani yanatumika kurekebisha kiwango cha sukari mwilini hasa kwa watu wenye tatizo la kisukari
- Unapunguza uvimbe na maumivu ya viungo
- Unaongeza kiwango cha maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha
- Unapunguza maumivu yanayotokana na mafua makali
- Unapunguza kiwango cha kolesteroli mwilini
- Mbegu za Mlonge hutumika kutengeneza mafuta yenye ubora sawa na mafuta ya alizeti na mzeituni
- Unaweza kutumika kutengeneza vipodozi kama sabuni na mafuta
- Maua ya mlonge hutumika kutengeneza chai ya mmea
- Unga wa majani ya Mlonge unapochanganywa na chakula huongeza nguvu mwilini
Kiwango cha Viinilishe katika Mlonge
i. Mmea wa Mlonge una kiwango cha Vitamin C mara saba zaidi ya machungwa
ii. Una kiwango cha Vitamin A mara nne zaidi ya Karoti
iii. Una Kalsiamu mara 4 zaidi ya maziwa
iv. Una madini ya Chuma mara 3 zaidi ya mchicha
v. Una madini ya Potasiamu mara 3 zaidi ya ndizi
vi. Majani ya mlonge yana kiwango cha protini mara mbili zaidi ya maziwa
Viinilishe vyenye Faida kwa watoto (Mlonge unaitwa “Rafiki Kipenzi wa Mama)
Gramu 25 za unga wa majani ya Mlonge zinaweza kumpa mtoto mchanga viinilishe vifuatavyo:
i. Asilimia 42 ya kiwango cha Protini kinachohitajika kwa siku
ii. Asilimia 125 ya kiwango cha Kalsiamu kinachohitajika kwa siku
iii. Asilimia 61 ya kiwango cha Magnesium kinachohitajika kwa siku
iv. Asilimia 41 ya kiwango cha Potasiamu inayohitajika kwa siku
v. Asilimia 71 ya kiwango cha madini ya Chuma kinachohitajika kwa siku
vi. Asilimia 271 ya kiwango cha Vitamin A kinachohitajika kwa siku
vii. Asilimia 22 ya kiwango cha Vitamin C kinachohitajika kwa siku
Unapolima Mlonge una nafasi kubwa zaidi ya kuongeza kipato na pia kuboresha lishe. Sehemu zote za mmea wa Mlonge zina uwezo wa kuongeza kinga ya mwili.
Matumizi Mbalimbali ya Mlonge Kusafisha Maji
i. Kusanya mbegu za Mlonge zilizokomaa kisha zimenye kupata kiini
ii. Twanga kiini mpaka upate unga
iii. Weka gramu 2 (vijiko viwili vya chai) za unga
wa mlonge kwenye maji kiasi (nusu lita) na tikisa kwa muda ili kupata mchanganyiko mzuri
iv. Changanya kwenye maji lita 20 na koroga sana kwa muda wa dakika 10-15
v. Yaache maji yatulie kwa masaa 2 juani, utaona uchafu umetuama chini
vi. Yachujie maji kwenye chombo safi na kisha yaweke juani masaa machache. Kwa njia hii,
kiwango cha madhara ya maji machafu kinapungua kwa asilimia 80-90. Inashauriwa kutumia kiwango cha miligramu 30-300 za unga wa mlonge kwa lita moja ya maji kwa Kuzingatia kiwango cha uchafu. Angalizo: Maji yachemshwe kabla ya kunywa.
Chakula cha Mifugo
- Majani ya Mlonge yanaweza kulisha ng’ombe, mbuzi, nguruwe na sungura. Yanaweza pia kutumika kulisha samaki katika mabwawa. Inashauriwa kupanda Mlonge karibu na bwawa la samaki.
- Mashudu ya mbegu za Mlonge yanaweza kutumika kama mbolea zenye kiwango kikubwa cha Naitrojeni.
- Maua ya Mlonge ni mazuri kwa chakula cha nyuki katika uzalishaji wa asali, hivyo inashauriwa kupanda
- Mlonge katika maeneo yenye mizinga ya nyuki Kuchanganya na mazao mengine
- Kutokana na mmea wa Mlonge kuwa na mizizi mirefu isiyosambaa na hauna kivuli kikubwa; unaweza kutumika kuchanganya na mazao mengine yanayohitaji kiwango kikubwa cha Naitrojen
- Mbolea ya MajaniNMaji yanayotokana na majani ya Mlonge yanaweza kutumika kama mbolea ya majani kwani yana uwezo wa kuongeza uzalishaji kwa asilimia 30
- Majani ya Mlonge yana virutubisho muhimu kwa utengenezaji wa Biogas
- Mbolea ya Kijani
- Mlonge ukipandwa kwa wingi kisha ukachanganywa kwenye udongo, unafanya kazi kama mbolea ya asili
- Kuzuia magonjwa ya mimea
- Kuchanganya majani ya Mlonge kwenye udongo kabla ya kupanda husaidia kuzuia ugonjwa wa kiuno (damping-off) unaoshambulia shina la mmea
- Jinsi ya Kuandaa Mlonge kwa Matumizi Mbalimbali
- Majani mabichi ya Mlonge
- Tumia majani ya Mlonge usiokomaa au majani machanga toka mti uliokomaa. Inashauriwa kuongeza
- majani ya Mlonge wakati wa hatua za mwisho za mapishi ili kutoharibu viinilishe muhimu yaani vitamini na madini
- Ili Kutengeneza supu ya majani, majani yaliyokaushwa yanaweza kutumika badala ya majani mabichi.
- Vuna majani ya Mlonge toka mtini
- Yaoshe kisha yaache yakauke sehemu isiyo na jua (ukianikwa juani virutubisho hupotea).
- Yatwange majani yaliyokauka ili kupata unga wa Mlonge.
- Utunze unga wa Mlonge kwenye chombo kikavu chenye mfuniko sehemu isiyo na joto
- Ongeza vijiko viwili vya Mlonge kwenye chakula au mboga ili kuboresha lishe
- Maua yana kiwango kikubwa cha madini ya Kalsiamu
- Ni lazima yachemshwe kabla ya kuliwa
- Mbegu za Mlonge hutumika kupunguza homa
- Zinapoliwa mara kwa mara zinaulinda mwili usipatwe na magonjwa mbalimbali mf. Mbegu nne za mlonge zikiliwa kila siku (mbili asubuhi, mbili jioni) zinasaidia kupunguza maumivu ya viungo na
Mafuta ya mbegu za Mlonge
Mafuta ya Mlonge yanasaidia sana kupunguza maumivu na uvimbe
i. Acha mbegu zikauke zikiwa mtini ndipo uvune
ii. Kama hazijakauka zianike juani
iii. Ondoa ganda la mbegu ya mlonge kupata kiini.
Source:Muungwana
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment