"FAIDA KIAFYA" ZA APPLE, NDIZI MBIVU, MAHARAGE, KABICHI, KAROTI, KAHAWA NA VYAKULA VYA NAFAKA.




APPLE (Tufaha)
 
• Dawa nzuri ya ugonjwa wa moyo 
• Hushusha kolestro 
• Hushusha shinikizo la damu 
• Huimarisha kiwango cha sukari katika damu 
• Huongeza hamu ya kula 
• Linakemikali yenye uwezo wa kuzuia saratani 
• Juisi yake inaua virusi vinavyoambukiza magonjwa 

BANANA (NDIZI MBIVU)
 
• Huzuia na kutibu vidonda vya tumbo 
• Hushusha kolestrol katika damu 

BEANS (MAHARAGE YA AINA ZOTE) 
• Hupunguza aina mbaya ya mafuta mwilini 
• Hudhibiti kemikali mbaya za saratani 
• Hudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu 
• Hushusha shinikizo la damu 
• Hurekebisha mwenendo wa utumbo mkubwa 
• Huzuia na kutibu ukosefu wa choo 
• Huzuia kutokwa damu kwenye haja kubwa (haemorrhoids) na matatizo mengine ya tumbo 

CABBAGE (KABICHI) 
• Hupunguza hatari ya kupata saratani, hasa ya utumbo 
• Huzuia na kutibu vidonda vya tumbo (hasa juisi yake) 
• Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili 
• Huua bakteria na virusi mwilini 
• Huharakisha ukuaji wa mwili 

CARROT (KAROTI)
 
• Inaaminika kuzuia saratani, hasa zitokanazo na uvutaji sigara, ikiwemo saratani ya mapafu. 
• Hushusha kolestro katika damu 
• Huzuia ukosefu wa choo (Constipation) 

COFFEE (KAHAWA)
 
• Kahawa si kinywaji cha mtu kupendasana kutumia, lakini kinapotumiwa kwa kiasi kidogo na kwa tahadhari, kina faida zake: 
• Huboresha utendaji kazi wa ubongo 
• Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa asma (asthma) 
• Hutoa ahueni kwa wenye homa 
• Huongeza nishati ya mwili 
• Huzuia meno kuoza 
• Ina kemikali ambayo huzuia saratani kwa wanyama 
• Hutoa uchangamfu 

CORN (NAFAKA- MAHINDI, MCHELE, N.K)
 
• Zina aina fulani ya kemikali ambazo huzuia saratani 
• Hupunguza hatari ya kupatwa na aina fulani za saratani, magonjwa ya moyo na kuoza kwa meno 
• Mafuta yake hushusha kolestro mbaya mwilini.

Source:Muungwana

Designed by CHAX C

Comments