"DIAMOND PLATINUMZ" AWASHUKURU MASHABIKI WAKE KWA KUMPA SUPPORT KWENYE VIDEO YAKE YA "I MISS YOU".



Baada ya kuachia video ya wimbo wake wa ‘I Miss You’ ambayo iliwahi kuvuja muda mrefu kidogo, Msanii wa muziki kutoka 255 Diamond Platnum ameonesha kufurahia views wanaoitazama video hiyo mtandaoni.

Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameonesha wazi wazi furaha hiyo na kuwashukuru mashabiki wake kwa kuitazama video hiyo kwa kuandika

 “611,054 Views within a Day and few hours….Views Laki sita na kumi ndani ya siku Moja na Masaa….. Eish! Nyie Mafans Mie Nawapenda Ujue jamani

#IMissYou,”


Hata hivyo ngoma hiyo imezidi kutikisa mtandao wa YouTube kwa kushika video namba moja inayo’trend kwa sasa huku ikiiacha mbali ngoma yake mpya ya ‘Fire’ aliyomshirikisha Tiwa Savage kutokea nchini Nigeria ambayo nayo ilitoka siku moja na ‘I Miss You’

Source:Bongo Newz

Designed by CHAX C

Comments