Ajali hii imetokea barabara ya Wiyenzele kuelekea chipogoro mtu mmoja amepoteza maisha hapo hapo. Aliyefariki ni mshabiki maarufu wa timu ya Yanga, anaitwa Ally Yanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha kifo cha shabiki maarufu wa klabu ya soka ya Yanga, Ally Yanga kilichotokea Jumanne hii katika ajali ya gari aina ya Rav4 eneo la Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Ally Yanga ambaye pia ni mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya Faidika ambalo lilikuwa kwenye promotion na sio kwamba alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama ilivyoelezwa hapo mwanzo.
Klabu ya Yanga imesema kifo cha shabiki huyo kimeacha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa pamoja na kuwa balozi mzuri kama mwananchama wa timu hiyo.
Marehemu atakumbukwa kutokana na mbwembwe zake alizokuwa akizionesha anapokuwa uwanjani na nje ya uwanja hasa pale timu yake inapokuwa katika mchezo.
Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo.
Source:Muungwana
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment