ASANTE "EDEN HAZARD" UMENITAFUTIA "MACKY CHRISANTUS"



18 August 2007 mjini seol-korea kusini ilizinduliwa michuano ya kombe la dunia ya soka kwa vijana wenye umri chini ya miaka17,tamati ya michuano hii ilifikia 9 September ya mwaka huo na kushuhudia Nigeria wakitwaa ubingwa wao watatu (kwa wakati huo) katika historia ya michuano hiyo..
Nikuambie kuwa katika michuano ile.. Eden Hazard na Christian Benteke walishiriki wakiichezea Ubelgiji ,Mamadousakho na ufaransa, Danny Welbeck na Victor Moses walikuwa wakiitetea England, Tony Kroos alikuwa akiiongoza ujerumani kama nahodha, Mapacha Fabio na Rafael da Silva walikuwa wakiipigania Brazil ….lakini hao wote walishindwa kuzifikisha timu zao fainali Ya michuano ile…  Nigeria ikatwaa ubingwa kwa kuifunga Hispania ya David De Gea kwa mikwaju ya penalty 3-0…..usishangae ni huyu huyu De gea mlinda mlango bora wa ligi kuu England misimu mitatu mfululizo.. siku ile aliziokota tatu kwenye wavu wake
Picha limeanza hapa……wakati Eden Hazard akitajwa kuwa moja ya wachezaji mahiri kabisa ligi kuu England huku akimfanya Florentino Perez akune kichwa kuvunja benki ili akamsaidie CR7 kufunga magoli,nimelikumbuka jina hili.. MACKY (Macauley) CHRISANTUS, siku mbili baada ya kuanza michuano ile alitimiza umri wa miaka 17,achana na hao niliokutajia hapo juu huyu alikuwa moto wakuotea mbali kwenye hayo mashindano..

 Eden Hazard
                                                                 
Aliiongoza Nigeria kutwaa Ubingwa ule huku akitwaa kiatu cha dhahabu na magoli yake 7..huyu ndiye alikuwa habari ya yale mashindano na maajabu yake yaliifanya klabu ya hamburgs vya ligi kuu Ujerumani imsajili na moja kwa moja akaingia kikosi cha wakubwa mwaka 2008….baada ya hapo habari zake hazikusikika tena sio kuhusu klabu anayocheza wala hata timu yake ya taifa….baada ya kuchoshwa na tetesi za Hazard kwenda Réal, nimeamua kupoteza muda wangu nakumtafuta,..ndiyo ni kwanini Hazard na siyo Chrisantus ???

Macauley Chrisantus
                                                       
 Hatimaye nikampata ..nimempata kule aliko kijana wetu Farid Mussa,ni ligi daraja la kwanza Hispania (Segunda Division) anaitumikia CF Reus Deportine kabla ya hapo alitolewa na Hamburg kwa mkopo katika timu za madaraja ya chini Ujerumani kwa misimu takribani mine na baadaye akaibukia Las Palma Sakakaa 2012-2014 na baadaye akapitia Sivarsport ya Uturuki kwa msimu wa 2014 -2015….nimeahirisha kumcheka ila imebidi nijaribu kuukubali ukweli na kuukataa uongo ya kuwa jamaa“kazingua” ,mastraika aliowanyoosha miaka tisa iliyopita huko Korea Kusini ndio hawa ambao kila jumamosi mimi na marafiki zake wa pale Lagos tunaenda kuwaangalia kila wikiendi… nikimaanisha Eden Hazard, Christian Benteke, Dany Welbeck..napia Victor Moses, 
Huyu Toni Kroos naye juzi tukaweka rekodi na real Madrid …sijaamua kuhangaisha akili yangu sana kutafta tatizo ya kwamba ni kwanini Chrisantus ameshindwa kuiteka Dunia ili hali mwanzo wake baada ya ile michuano ya vijana ulikuwa mzuri sana… nikaamua kuiangalia picha yake… nimetumia sekunde 30 tukujua tatizo.. nimegundua ni kwanini kina Hazard leo wanataka kushindana na akina Ronaldo huku yeye akishindana na akina Farid Mussa.

  Macauley Chrisantus (katikati), akiwa na Toni Kroos (kushoto) na Bojan Krkic (kulia).
   Picha ya pamoja baada ya utoaji Tuzo za mashindano ya Kombe la Dunia chini ya miaka 17                                           mwaka 2007 nchini Korea Kusini       

Kwa mujibu wa Google Macauley Chrisantus ana miaka 26 sasa lakini picha yake imemsaliti… imeamua kuongea ukweli… imeusaliti pia uongozi wake wa kwenye yale makaratasi ambayo NFF waliwapelekea FiFA mwaka 2007 yakiwa na vielelezo vyake ikiwemo mwaka wake wakuzaliwa… nchi za magharibi haswa Nigeria zimekuwa zikiupenda sana mchezo huu wa kudanganya umri kwenye timu zao za vijana..Pata muda uitafute picha ya muonekano wa Macauley Chrisantus leo hii na umri wake “wa Google “ wa miaka 26…hautaamini jinsi ambavyo anaonekana kuwa na miaka30 au zaidi,yaweza kuwa kipindi anawatesa kina David de Gea kwa mikwaju yake alikuwa na miaka ishirini na moja.. Nikirejea mechi ya fainali ile goli kipa wa Nigeria Dele Ajiboye alikuwa shujaa kwakupangua penalty mbili na moja kutoka nje.. kama ilivyokuwa kwa Chrisantus huyu naye aliibuka nyota wamashindano yale lakini leo haijulikani alipo…. Hayupo hata Notingham Forest ya daraja la kwanza England ...mwonekano wake hata wakati wa mashindano yale ulionyesha kuwa palikuwa na walakini kwenye umri wake halisi..alionekana mkubwa kuliko Ramadhani Kabwili waSerengeti boys..wale makipa watoto akina De Hea (Hispania) na Kevin Trapp (Ujerumani)  leo tunawaona Man Utd na PSG…hawa walikuwa watoto haswa na ndio maana imekuwa sahihi wao kufika hapa na niwakati sahihi kwao,safu ya ushambuliaji ya Hispania iliongozwa na Bojan Krkic ambaye leo yuko Stoke City baada ya kupita Barcelona, AC Milan , Ajax na bado anakimbiza..hali hii ya wachezaji kudanganya umri imewafanya wachezaji wengi wanaowika katika mashindano ya vijana kupoteza haraka ubora wao ukubwani huku “Google “ ikiendelea kuwabeba kwa kuwatambua kuwa bado ni vijana…
Rudi nyuma kidogo umkumbuke Nwanko Kanuna Michael Essien,wakati Steven Gélard anaondoka Liverpool kwenda Marekani na Miaka yake 35 tiyari Essienna Nwanko walishawahi kuondoka EPL na miaka yao 31 ya “Google “ …sasa kuna hii story ya John Obi Mikel …huyu inasemekana (kwa mujibu wa Google) ana miaka 30 na tiyari ametimkia ligi ya China.. Aliwahi kusema kwamba utotoni alipata kucheza soka na marafiki zake wakubwa wanamuziki pacha“P square “ wa Nigeria ,hawa wenzie kwasasa wana miaka 34, jaribu kufikiri kuwa kwa waafrika ninadra sana watoto wasio warika moja kuwa naukaribu wa kirafiki na kucheza pamoja…na hata hilo John Obi mikel sio jina lake sahihi… Jina lake halisi la wazazi wake anaitwa John Obinna Michael na inadaiwa lilikosewa na chama cha soka Nigeria wakati wakutuma majina ya kikosi cha U-17 kwenda FiFa kuelekea mashindano ya mwaka 2005…kama sio mpango wao inawezekana vipi shirikisho likakosea majina yote matatu????????
Kina Hazard wanatuonyesha kuwa wakati ule walishindwa kuwika mbele ya vijeba wa Nigeria ndio maana leo wanatamba katika muda sahihi na umri sahihi kabisa ……..
**UMRI**

Written by MWANAMAYEKA

Designed by CHAX C

Comments