Hauhitaji elimu kubwa sana ambayo haina uwezo wa kubadilisha maisha yako, elimu bora ambayo unaihitaji au unatakiwa uipate ni elimu ya kubadilisha maisha yako, elimu ambayo itakunyanyua au kukutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine kimaisha. Mafanikio yako makubwa yanakuja kwa kujipatia elimu inayotoa thamani ya maisha yako na sio vinginevyo.
Kwa hiyo kama kwa namna moja au nyingine umekosa elimu kubwa ya darasani na kufika mahali unajilaumu kwamba ningesoma ningefika mbali sana kimafanikio, unakosea, huu sio wakati wa kusikitika. Jifunze kutafuta elimu yenye thamani itakayobadilisha maisha yako. na habari njema ni kwamba elimu hiyo haipatikani darasani, inatafutwa mtaani kwa watu sahihi.
Ni mzigo mkubwa sana kwako na kwa jamii kwa ujumla kuwa umesoma halafu hauna mafanikio makubwa. Kama iko hivyo kwako, jiongeze kidogo tu, anza kuisaka elimu sahihi, elimu ambayo itakupa thamani sahihi ya maisha yako na kukubadilisha na kuwa mtu wa mafanikio. Maisha ya mafanikio hayaji kwa kusoma saana, bali ni kwa kujifunza vitu sahihi ambavyo vina uwezo wa kubadilisha maisha yako.

Source:Muungwana
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment