JINSI YA KUZUIA MTU KUHACK AKAUNTI YAKO YA INSTAGRAM


 

"Njia za kawaida"

      Hakikisha unatumia password ngumu yenye mchanganyiko wa alama, namba, pamoja na herufi, pia ni vyema kutumia alama hizi (! na &) kwan zinaongeza ugumu pamoja na kudumu kwa password yako.

       Badilisha password yako kila mara hasa pale unapoona meseji kutoka instagram ikitaka ufanye ivo, Hii ni muhim sana kwani instagram hupendelea kutuma meseji hizo pale wanapoona akaunti yko inadalili za kuhackiwa.

       Hakikisha email yako iko salama kwani mtu yeyote mwenye uwezo wa wa kuingia kwenye email yako basi pia mtu huyo anauwezo wa kuhack akaunti yako.
   
     Hakikisha  una logout pale unapotumia sim au kompyuta ya mtu kuangalia akaunti yako.

       "Njia za muhimu"

    Hakikisha unaweka namba yako ya simu kwenye akaunti yako kwani mara nyingi namba hii inaweza kukusaidia kurudisha akaunti yako iliyo hackiwa.
   
     Hakikisha hautumii password sawa na email yako au mahali pengine popote, kifupi hakikisha unatengeneza password kwa ajili ya instagram pekee zisifanane na password unazotumia popote.

      Hakikisha unawasha sehemu maalumu ya "Two-Factor Authentication" sehemu hii itakusaidia kutumia password maalumu pale unapotaka kuingia kwenye kifaa tofauti na sim yako.

   Ili kuwasha sehemu hii nenda kwenye profile yako kisha bofya settings kisha utaona sehemu iliyoandikwa "Two-Factor Authentication" bofya hapo kisha set sehemu hiyo kwa kutumia  simu yako.

     Hakikisha unazuia matumizi ya akaunti yako ya instagram kwenye program zingine kwa mfano unakuta mahali unaweza ku login kwa kutumia akaunti yako ya instagram ili kulinda akaunti yako. Usipendelee kufanya hivyo badala yake tumia njia za kawaida za kujisajili kwenye akaunti mbalimbali mtandaoni








Picha hizi zinaonesha namna ya kuweka password maalumu kwa kuzuia akaunti yako isiibiwe(kuhackiwa),Utakuwa unaitumia kila unapoingia kwenye akaunti yako ya Instagram.
Nenda Profile yako>option(setting)>Two Factor Authentication>Turn on>Set Password yako.
Hakikisha password yako isifanane na ya Email yako pia hakikisha unachanga alama hizi ! & @ , Password yako itakuwa strong.
Itakuwa vigumu kuhackiwa.

                      "Hitimisho"
"Hacker hutumia akaunti zako zingine kuweza kujua Password zako,hivyo sijambo la muhimu kutumia Password zinazofanana na akaunti zingine zozote za mitandaoni.

  Asanteni kwa ushirikiano wenu.

Designed by CHAX C


Comments