Somo hili linahusu jinsi ya kuchukua 'screenshot' kwenye kompyuta. Mara nyingi watu wanaweza kuchukua screenshot kwenye simu zao kwa kubofya batani za volume up +power off (kwa baadhi ya simu.). Ila hapa utajifunza jinsi ya kufanya hiyo screenshot kwenye kompyuta ila ni kwa wale wanotumia operating system ya windows.
Njia mojawapo ya kuchukua screenshot ni kutumia program inayoitwa 'snipping tool'. Fata hizi hatua zifuatazo:-
1. Nenda kwenye window kisha search kwa kuandika neno 'snipping tool' baada ya hapo utaibofya hiyo program iliyojitokeza.
2. Baada ya hapo hiyo program ikisha jitokeza uta-drag sehemu ambayo unayoitaka kuchukua 'screen shot'.
Kisha utaenda sehemu iliyoandikwa file, save na andika jina unalohitaji. Hapo utakuwa tayari umeshachukua screenshot kwenye computer.
AU
Hii ni njia nyingine lakin hii ni ya kuchukua screen yote, hakuna 'option' ya kuchukua sehemu ya screen. Hapa ni katika keyboard yako mara nyingi huwa kwenye batani za juu kulia kuna batani imeandikwa 'PrtScr' ukiibofya hiyo utakua umechukua picha ya screen ya yote.
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment