Akifanya interview moja nchini humo, licha ya kutotaka Tiffa awe mwanamuziki Diamond amesema pia kuwa atafurahi zaidi kama mtoto wake wa kiume akiwa staa wa muziki kama yeye.
“Mwanamke ni kweli anatongozwa na watu tofauti ila unapokuwa msanii unajulikana na wengi kwahiyo ukijulikana na wengi kutongozwa kuna kuwa kwingi pia sasa wataniuwa kwa pressure.” – Diamond.
Aidha, katika interview hiyo Diamond aliugusia pia kuhusu kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zari ambaye sasa ni mpenzi wake, Ivan Semwanga ‘Ivan Don’ aliyefariki dunia siku chache zilizopita akisema haikuwa rahisi kuahirisha show akisema akitoka kwenye show Kenya atapitia Uganda kwenye mazishi hayo kabla ya kurudi Tanzania.
“Ilikuwa ni wakati mgumu na nilikuwa nimewekewa oda na msiba ukawa umetokea kwahiyo ku-cancel ghafla show ya watu inaweza ikawa taswira tofauti, sikuwa na jinsi lakini niliongea na mzazi mwenzangu akanielewa….. nikimaliza show hapa nitaenda Uganda kuzika halafu nitarudi nyumbani.” – Diamond.
Source:Muungwana
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment