MWANAMITINDO na video queen mwenye umbo tata Bongo, Jane
Rimoy "Sanchi" amefunguka kuwa thamani yake ni kubwa hivyo mwanaume anayetaka
kumuoa lazima ajipange kwa mahari ya milioni 10 za Kitanzania.
Akizung-umza na Star Mix, Sanchi
mwenye figa matata alisema kuwa, siku zote wanaume wanaowaoa wanawake kwa
mahari ndogo huwachukulia hivyohivyo lakini akilipa mahari kubwa hata heshima
inakuwepo na uthamini pia.
“Unajua mwanaume wa kweli
unampima kwenye vitu vidogo kama hivyo, mimi mahari nataka iwe ya heshima
kabisa na kama mtu hana milioni hiyo 10 basi hana sifa ya kuwa mkewe na
kunimiliki,” alisema Sanchi.
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment