Hit maker wa Aje, Alikiba baada ya kufanya kazi na kampuni ya usimamizi wa kazi zake ya Rockstar4000 kwa takriban miaka 6, Jumatatu hii ametangazwa rasmi kuwa mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Rockstar4000, Muimbaji
huyo amekuwa mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo, pia ni Director of
Music and Talents.
“King
Kiba alitangazwa rasmi kuwa sehemu ya wamiliki wa Kampuni ya Rockstar4000 Music
Entertainment Co & Rockstar Television,” Ilisemwa Taarifa hiyo kwenye Media
mbalimbali.
“Ali
kiba kwa sasa amekuwa sehemu [Kiongozi] wa wasanii walio chini ya Rockstar4000
pia ni Director of Music And Talents,”
Rockstar
Television inajishughulisha na Utengenezaji wa vipindi vya mastaa tofauti
kutoka nchi mbalimbali na kuvisambaza katika vituo vya Television vya
kimataifa.
Kwa
sasa nchini Tanzania kampuni hiyo inamsimamia “Baraka The Prince”,
“Lady Jay Dee” pamoja na yeye mwenyewe[Ali Kiba].
BY CHAX C
Comments
Post a Comment