MREMBO "GIGY MONEY' ATOA POVU KUHUSU LENZI ZA MACHO ZA "WEMA SEPETU".

Baada ya kuambiwa ameiga kuweka lenzi katika macho yake ili avutie, Gigy Money ameamua kutoa povu kwa wale wanaomwambia ameiga kitendo hicho kutoka Wema Sepetu.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram mrembo huyo asiyeishiwa na vituko ameporomosha mapovu hayo kwa kuandika.
“Yani kuna watu wengine makubwa jinga etiii kabisaaa kisa lens za macho tena bandia watu wanapaniki mm mtu wa ajabu kwel cos nimeamua kuvaa miwani tu lens vaaeni nyie muwe vibonge kama zinanenepesha #kuwafakehakujawaikumuachamtusalama #bilakisahausiwaogopi ,” ameandika Gigy.
Ameongeza “Povuuuu linaruhusiwa kwanza mnasemaga hakuna wakunijibu sasa alie nijibu ni wema rapper sijuiii?
alafu nyie timu yake waswahili sana yani wengi wenu mnatokea magomen keko na mwananyala so hamniboi cos mm mwenyewe mtoto wa kurasin so byeeeeeeeeeeee bythiiiiizzzzss pia anaecoment ananikubal kama hunikubal pita kimyaaaaa.”

BY CHAX C

Comments