Skip to main content
TAZAMA UTOFAUTI WA "ASLAY" KATIKA MUZIKI KWA SASA.
Baada ya uongozi wa kundi la Yamoto Band kutoa fursa
kwa kila msanii kufanya kazi zake binafsi.
msanii Aslay ameeleza mabadiliko
katika maisha yake ya kimuziki.Muimbaji
huyo amesema hayo kupitia XXL ya Clouds FM kwa sasa anamiss kukaa na mwenzake
kwa muda mwingi kama ilivyokuwa mwanzo na hata kuonana ni kwa mara chache kwa
kuwa kila mtu anakuwa bize na mambo yake.
Katika hatua nyingine Aslay ameongeza
kuwa si kweli kwamba kwa sasa anatafuta mashabiki wake wapya katika muziki wake
kwa sababu alishatengeneza njia nzuri akiwa Yamoto Band“Nasonga vizuri tu,
najiona kuna upya fulani lakini si wa ku-hustle wa kuwafikia tena mashabiki,”
alisema "Aslay".
Source: Bongo Newz
Comments
Post a Comment