STAR "WASTARA" NA SKENDO NZITO YA "RUSHWA YA MAPENZI".




MSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma amerushiwa skendo nzito ya Rushwa ya Mapenzi baada ya kuvujishwa kwa ‘chatting’ yake na jamaa mmoja anayedaiwa kuwa na pesa chafu ‘Pedeshee’ aliyefahamika kwa jina la Patrick.
Limekujaje hili
Awali akifanyiwa mahojiano na gazeti hili kuhusiana na maisha yake ya kimapenzi, Patrick ambaye ni msanii wa muziki ambaye naye alikuwemo kwenye orodha ya mastaa wa madawa ya kulevya alisema kuwa, huko nyuma aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wasanii mbalimbali lakini aliachana nao baada kutofautiana.



Miongoni mwa mastaa aliowataja ni pamoja na Wastara, Johari na wengine ambapo kutokana na maelezo yake hayo, gazeti hili liliona ni vyema kupata uthibitisho wa kile alichokisema kabla ya kuandika gazetini.
PATRICK ATOA USHAHIDI
Baada ya kubanwa sana ikiwa ni pamoja na kuambiwa kuwa anatafuta kiki kwa kudai alitoka na mastaa hao wakati hana jeuri hiyo, Patrick alimfowadia paparazi wetu ‘chatting’ aliyokuwa anafanya na Wastara kupitia Mtandao wa WhatsApp wakati walipokuwa wapenzi.


Kwenye ‘chatting’ hiyo zilionekana baadhi ya meseji ambazo zilikuwa chafu hali iliyomfanya mwandishi azitilie mashaka kama kweli zil­itoka kwa Wastara kwenda kwa mwanaume huyo ama kuna kitu kinaendelea.
Baada ya kupata madai hayo ya Patrick na ‘chatting’ ambayo ‘ameikapcha’ kwenye simu yake iliyokuwa sambamba na picha na video romantic za Wastara, alizo­dai kuwa alikuwa akimtumia jamaa huyo, mwandi­shi wetu aliona ni busara kumtafuta Wastara ili aifun­gukie skendo hiyo nzito iliyomganda.




Alipopatikana kupitia simu yake ya mkononi alifun­guka hivi: “Huyo mtu simjui na picha nimeziona wamezitengene­zatengeneza tu kwa maana haku­na picha yoyote ambayo labda kusema nimekaa naye nipo utupu ama kuna kitu nafanya naye. Huyo mtu anatafuta kiki kwani ame­shamchokonoa kila mtu na wote wamemkimbia.

“Sina mazoea naye yoyote zaidi ya siku moja kunitafuta na ku­niambia anataka kutengeneza video ya muziki akaja kuniletea vitu vingine tokea hapo nikamji­bu mbaya. Kama kuna video ipo nimemtaja jina lake sawa ila ninachojua hakuna kitu kama hi­cho.
“Nilishamtukana asinizoee! Sijaishi katika mazingira hayo, sijapata ustaa kwa kuchati na wa­naume, iweje mtu aje kuniharibia jina langu nililotengeneza kwa miaka mingi. Sijap­endwa na watu kwa kukaa utupu.”


Source: Raha za Walimwengu


Designed by CHAX C

Comments