Muigiza Aunt Ezekiel amesema Bongo Movie haijafa ila ni muda wao wa kupumzika ili kujipanga.
Mrembo huyo amefafanua kuwa hiki ni kipindi cha wao kujipanga na wale wanaofikiri Bongo Movie haitarejea katika kiwango chake wanakosea.
“Bongo Movie tunaweza kusema ni kama maisha ya binadamu, kuna time analala, anaamka, anapika, so kunakuwa na kazi tofauti tofauti. Naweza kusema kwa sasa hivi Bongo Movie ni muda wetu wa kurelax kwanza kwa hiyo tumepumzika, tumelala tukishaamka nadhani tutakuja na vitu vingi vya tofauti,” Aunt Ezekiel amekiambia kipindi cha Twenzetu cha Times FM.
“Sio kwamba tukilala ndio hakuna kitu ambacho kitakuja kikubwa zaidi au hakitachukua akili za Watanzania tena, hapana kulala kwa Bongo Movie ni kulala kwa kujipanga ili tunapokuja kurudi tena turudi vizuri, so mimi siamini kama Bongo Movie imekufa, tumerelax tu,” ameongeza.
Source:Raha za Walimwengu
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment