- Msanii wa Bongo Fleva kwenye Lebo ya WCB "RAYVANNY" jana Usiku alishinda Tuzo ya BET Viewer's Choice Best New International Act 2017,
- Kwa Tukio hilo kubwa la jana Limemfanya "Rayvanny" akumbuke mbali Kimaisha, tokea alipoanza Muziki akiwa TIP TOP CONNECTION kwa Madee,hata hivyo amemshukuru sana "Madee" kwani ndio alikuwa mtu wa karibu pindi anapokwama katika shughuli zake ikiwamo MUZIKI.
- Hatimaye leo "Rayvanny" amefunguka kwa kusema;
- "Nakumbuka Miaka Sita Iliyopita ndio kipindi ambacho nilikutana na Madee.Kipindi hicho Sikujua nilichonacho pia sikujua Wapi nianzie na nini nifanye.
- Kilikua kipindi kigumu sana Kwangu sababu nilikua Mgeni Dar as salam.Lakini kaka angu Madee alisimama na mimi Kila alipokua akienda alienda na mimi na hii yote ni baada ya kuniona mnyonge nisie na msaada.Nilijuana na Wadau na baadhi ya wasanii Kupitia kaka angu.
- Madee Pia alikuwa akinipeleka studio na kunishauri Vitu vingi sana vya kimaisha na muziki pia na kusisitiza kuwa Nisikate tamaa.
- Nimepata Uzoefu Mkubwa wakutumbuiza mbele ya kundi la watu kutoka kwake.Kuna kipindi nilikosa hata Nguo za kuvaa alikuwa akinipa hata nguo alizokua akizipenda yote kunistiri mdogo wake.
Nakumbuka kuna kipindi Akasema "mdogo wangu Ray, jifunze gari",nikamkatalia nakumwambia kwamba mimi nitaendesha Wapi gari na Nitakuja lini kupata gari.Akaniambia mdogo wangu Una kitu ambacho kitakusaidia baadae yote yatawezekana.
- Alianza kunifundisha Gari yake japo nilikua naigongesha gongesha kwenye mashimo sababu nilikua sijui lakini alinivumilia hadi nikajua.Pia Nikawa mjanja wa vitu vingi na kujiamini kisa yeye.
- Siku Nilipomwambia Naenda Wasafi nilijua hatonielewa Lakini Ndio alikuwa mstari wa mbele mambo yangu yafanikiwe nae akichangia mpaka "Raymond tiptop" akawa "Rayvanny".
- Hadi leo Hii Tumechukua Tuzo kubwa duniani "BETA wards"
- MUNGU AKUBARIKI KWA MOYO HUO HUO SINA CHA KUKULIPA MUNGU PEKEE NAKUSHUKURU WEWE NA FAMILIA NZIMA YA SENEDA.... HUU MWANZO MUNGU MWEMA Alisema "RAYVANNY"
WRITTEN AND DESIGNED BY CHAX C
Comments
Post a Comment