PICHA: UTAUPENDA MUONEKANO WA "BEN POL" NA "EBITOKE",- WADAI ETI WANAPENDANA NA KUANDIKIANA UJUMBE HUU.
Nini kinaendelea kati ya Ben Pol na Ebitoke? Wawili hao wamepiga picha wakiwa pamoja hali iliyoleta maswali mengi kwa mashabiki kupitia mitandao ya kijamii.
Ebitoke ambaye ni mchekeshaji kutoka Timamu Media, wiki chache zilizopita aliweka wazi kwamba anampenda sana Ben Pol na kudai angenda kuolewa naye.
Naye muimbaji huyo wa R&B hakuonyesha kupingana na kauli ya mwanadada huyo kwa madai kuwa anaheshimu hisia zake.
Ijumaa hii mashabiki katika mitandao ya kijamii wamekuwa surprise baada ya wawili hao kupiga picha wakiwa pamoja na kila mmoja kupost na kuandika ujumbe wake.
Ben kupitia Instagram Ben Pol aliandika, “Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba kwa Mhusika? Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao, Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu duniani sisi sote TUNAPITA, na labda huyo Mtu kesho hatokuwepo. Ebitoke umenifundisha jambo KUBWA SANA maishani, najua wengi walikubeza sana , wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na Mimi.. lakini huwezi amini Mimi nimefurahi mno!! kukutana na wewe na kuongea, na nimepata jambo kubwa sana. Na Nitayaishi Maneno yako
. Nakushukuru sana, Mwenyezi Mungu akuzidishie. You are THE BEST
Source:Bongo Newz
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment