Msanii Barakah
The Prince amefunguka baada ya kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli siku chache zilizopita wakati akiwa katika
ziara yake katika Mkoa wa Pwani juu ya wanafunzi watakaopata mimba wakiwa
shuleni.
Rais Magufuli
alisema katika wa utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na
kuruhusiwa kurudi shule. Kutokana na kauli hiyo Barakah ameiunga mkono lakini
amemtaka Rais kuangalia upya kauli yake hiyo juu ya wanafunzi hao wa kike na
badala yake wanaume wanaowapa mimba watoto hao ndio wapewe adhabu kubwa zaidi.
Akiongea na Bongo5, hitmaker huyo wa Acha Niende amesema,“Japo kuwa ni
kweli hawa mabinti wakiwa wanarudi shule itakuwa ni system sasa ya mabinti wote
kubeba ujauzito kwa kuwa anajua hata nikibeba mimba nitakaa miezi tisa tu
halafu nitarudi darasani.
Hiyo ya kufukuzwa shule na asirudi kabisa hilo ni
funzo lakini sidhani kama ni plan ya Mhe. Rais, lakini itakuwa ni fundisho na
itawafanya watu wawe makini.”
“Watanzania tunaishi katika mazingira magumu sana ujue, mtoto katoka kwao
kapewa labda shiingi 500 tu ya nauli na hata hajui atapataje breakfast shuleni
halafu anaenda anakutana na vijamaa wanampa shilingi 50,000 au laki,
wanamshawishi mtoto wa watu anajikuta anaingia kwenye hayo mambo. Hawa jamaa
ambao ndio kishawishi kikubwa kwa hawa wanafunzi inabidi wachukuliwe hatua kali
sana,” aliongeza "Baraka Da Prince"
Wakati huo huo muimbaji huyo amesema yeye hajawahi kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mwanafunzi katika maisha yake.
Source : Bongo Newz
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment