FUNIKO : TAZAMA "MBWA" MWENYE SURA MBAYA KULIKO YOTE DUNIANI.

Mbwa huyo avunja Record ya kuwa na Sura mbaya kuliko Mbwa wote walioshiriki katika Mashindano hatimaye kuibuka mshindi katika Kinyang'anyiro hicho mpaka kuchukua TUZO.

Jina la Mbwa huyo anaitwa "Martha", ametajwa kuwa ni mbwa mwenye sura mbaya zaidi Duniani. Shindano la kila mwaka ambalo sasa liko katika mwaka wake wa 29 lilifanyika katika eneo la Petalum mjini Carlifornia."Martha" anayemilikiwa na Shirly Zindler aliwashinda wapinzani 13 na kupewa taji na pesa taslimu Dola 1,500.
Mbwa huyo mwenye taya kubwa sasa atasafirishwa hadi mjini New York kwa maonyesho ya vyombo vya habari kulingana na waandalizi wa shindano hilo.
Maonyesho hayo ya Sonoma Marin yanasema kuwa shindano hilo huwashirikisha mbwa wengi ambao wameokolewa katika makazi na maeneo ya kukuza mbwa kwa lengo la kuwauza.Mbwa mwenye sura mbaya zaidi Duniani.
"Martha ni Mbwa aliyeokolewa ambaye karibia awe kipofu kutokana na kupuuziliwa mbali,alisema "Bi Zindler".                                                                                                             
''Baada ya kufanyiwa upasuaji sasa anaweza kuona tena na hahisi uchungu wowote''.
Shirika la habari la AP limesema kuwa "Martha" aliibuka mshindi kwa kutembea katika ukumbi na kuwavutia majaji.
Majaji hao walimpatia ushindi mbwa huyo kutokana na hisia za watu, sura, tabia na hisia zake.
Designed by CHAX C


Comments