ANTONIO
CONTE :KUNA BOSI MMOJA TU CHELSEA
Mabilionea
wanaziamini sana BENKI kuliko hata walinzi wao binafsi (personal body guard),
bilionea anaamini BENKI ndiyo inalinda uhai wake, bilionea anaamini BENKI ndiyo
inampa thamani yake mbele za watu na siyo zile suti ghali za chapa adhimu ya Hugo
boss,wakati weweunaamini pesa huleta MAJIVUNO bilionea anaamini pesa huleta MAVUNO
kiasi kwamba yeye anamini zaidi kwamba hata akipanda miwa mbele ya pesa
haishindikani kuvuna mihogo… Hii ni hulka inayotawala fikra za mabilionea wengi
akiwemo Roman Abramovic….
Kuna
mtu mmoja anajaribu kucheza na akili za bilionea, anajaribu kutengeneza
shinikizo ili kumfanya bilionea amwamini yeye zaidi hivyo afanye analolitaka..
Mtu huyu anajaribu kujisahaulisha kuwa kitu pekee kinachoweza kumtengenezea
shinikizo bilionea na kumfanya apoteze walau usingizi mmoja kwa wiki ni BENKI
pekee ambako ndiko ubatizo wa jina lake ulifanyika.. Mtu huyu anaitwa Antonio
Conte, nashindwa kuelewa anachokifanya na anachokiwazakwa sasa muitaliano huyu,
Conte leo anahoji kwa nini hajapewa fungu kubwa la
usajili,wakati akiwa anahoji anataharuki zaidi baada ya kugundua kuwa pesa ya
usajili ipo lakini majukumu yote amepewa mkurugenzi wa ufundi Michael Emenalo..hapa sasa Conte anachanganyikiwa,
akili yake inamwambia kuwa amedharauliwa sana, akili yake inamwambia kuwa yeye
ndiye BOSS wa Chelsea kwa sasa kisa ametoka kuchukua taji miezi miwili tu iliopita, akili yake inaenda mbali zaidi na kumwaminisha kuwa
wakati huu alipaswa aachiwe PESA na afanye marekebisho ya kikosi kwa uhuru
wake.. akili yake inaamua kusahau kabisa kuwa hicho alichokuwa anakifikiri hata
Mourinho aliwahi kufikiri hivyo miezi kumi na tano iliyopita… Leo akili yake
inakuja na uamuzi ambao hata yeye anauafiki haraka haraka kuwa atingishe mguu, na
zaidi atingishe miguu yote miwili kwa kushirikiana na wakala wake kutengeneza
tetesi kuwa eti ametengewa maslahi mazuri pale Inter Milan kama Chelsea
hawatatekeleza matakwa yake kwenye usajili…… Sijawahi kuona msanii wa
vichekesho kutoka Italia ila Antonio Conte amenifanya nicheke sana…
anamtingishia miguu nani eti? Huyu huyu Roman Abramovic? Ulishawahi kumuona Abramovic akitabasamu
pindi Chelsea inapobeba ubingwa? Huyu jamaa hutoa matabasamu mawili kwa wakati
mmoja, tabasamu la kwanza ni kama lile la John Terry la kufurahia taji la 5 la
ubingwa wa EPL, tabasamu la pili ni lile la kuona msimamo na kile anachokiamini
siku zote vinazidi kulipa na kuzaa matunda vizuri pasina shaka , ni ule msimamo wake wa
kubadili makocha 12 ndani ya misimu 14hukutimu ikitwaa makombe 15 tangu awe
mmiliki wa Chelsea, Abramovic kama mfanyabiashara madhubuti haoni ajabu
kuchukua maamuzi ambayo machoni kwa wengi yanaweza onekana magumu japo kwake ni
rahisi tu kama kuvunja mkataba na kocha ndio maana anafurahi kuona kama Antonio
Contealiyemletabaada ya kumfukuza Mourinho anampa ubingwa basi hata siku
akimchukua Diego Simeone msimu ujao
pasina shaka atampatia ubingwa… hii ndiyo sababu anaamini yeye ndiye
BOSS wa Chelsea, anaamini ujanja wake wa kubadili makocha na kununua wachezaji
mahiri kwa kushirikiana na swahiba wake Michael Emenalo ndiyo umeifikisha Chelsea hapa ilipo
na siyo ujuzi wa makocha aliowahi kuwaajiri … Kwake yeye makocha huwaruhusu
wachukue cheo cha umanager na hayuko radhi kuwapa uBOSS, Mourinho alijaribu
kutaka kuiba uBOSS wake kilichompata anakijua… Conte anajaribu kutumia ubingwa
alotwaa juzi kama ngao wakati akijaribu shabaha ya kuzipiga fikra za mmiliki wa
timu anayofundisha ,Conte nakuomba utambue kuwa mrumi (Roman) abramovich hatingishiki
hata kidogo na hicho unachokiona wewe ni ngao ni sawa na boksi tu maana hata
muitaliano mwenzio Ancelotti alianza vizuri kukuzidi hata wewe lakini mataji
yake mawili yaliishia na barua ya kuachishwa kazi tena akipewa kwenye korido za
pale Goodison Park May 2011…Conte usidanganywe na hisia za mashabiki ukadhani
wanakuungamkono na hizo harakati zako ambazo zimekosa umakini kuzidiwa na zile
za Joram kiango wa Ben R. Mtobwa……Nimalize kwa kukupa hii lonja ya kuwa pale
Chelsea maBoss walikuwepo kipindi kile wewe unacheza soka ila tangu ustaafu
wanaoajiriwa ni maMeneja tu ukiwemo wewe pia…. Nikunong’oneze na hili japo
usimwambie mtu ni hivi kama ulikuwa hujui “role model wa Abramovic ni
Florentino Perez “
By
MwanaMayeka
Written by MWANAMAYEKA
Designed by CHAX C
Comments
Post a Comment